Na Amiri Kilagalila,Njombe

Wakurugenzi wa halmashauri za mkoa wa Njombe wamesema wapo tayari kuandaa ripoti zinazohusu leseni za vitalu vya madini visivyofanya kazi mkoani humo na kuwakabidhi wabunge ili kuwasilisha katika bunge kuona uwezekano wa kufuta umiliki wa vitalu hivyo.

Kupitia kikao cha ushauri mkoa wa Njombe (RCC) wakati wa kuchangia hoja,mkurugenzi wa halmasahauri ya wilaya ya Njombe Juma Ally amesema wapo tayari kuandaa taarifa za kutosha na kuwakabidhi wabunge ili kufikisha bungeni kwa ajili ya kuwafutia leseni wamiliki wote waliohodhi vitalu na kushindwa kufanya kazi.

Awali kaimu afisa madini mkoa wa Njombe Fredrick Gurenga wakati akisoma taarifa ya utekelezaji katika sekta ya madini alisema mkoa wa Njombe unaleseni nyingi za uchimbaji wa madini lakini hazifani kazi.

“Mfano Ludewa tuna leseni 201za uchimbaji mdogo lakini zinazofanya kazi ni 3 tu,ukija Makete kuna leseni 34 lakini zinazofanya kazi ni 4,Wangimg’ombe zipo leseni 20,na zinzofanya kazi ni 10 hususani kwenye mchanga,hapa Njombe zipo leseni 7 alikini zinazofanya kazi ni 6 walau”alisema Fredrick Gurenga

Aliongeza “Kwa ujumla tuna leseni 312 lakini zinazofanya kazi ni 30,ukija kwenye uchimbaji wa kati kama za kwenye liganga na mchuchuma tuna leseni 4 na hizi zote hazifanyi kazi,kwenye leseni za utafiti ni changamoto kuwa zaidi kwasababu kuna leseni 68 na hakuna inayofanya kazi.Sisi tumeandika barua kwa wizara ya madini na tumependekeza maeneo yafutwe ili wapatikane wachimbaji wanaoweza kufanya kazi”alisema tena Gurenga

Naye mbunge wa Jimbo la ludewa Njombe wakili Joseph Kamonga,ameishauri serikali kufuta leseni za wamiliki wa vitalu vya madini wilayani Ludewa ambao hawafanyii kazi maeneo hayo ili kutoa nafasi na fursa kwa wachimbaji wadogo wenye uwezo  wa kuyaendeleza.                   

“Tumeshashuhudia kwenye Tanzanite tunapata Bilionea ambao wako jirani na mradi husika,pendekezo langu ni kwamba hizi leseni 201 zifutwe bila kumuonea aibu mtu yeyote,halafu watu wa madini wafike kwa wachimbaji wadogo wanaogundua madini kutokana na  kufukua fukua  ili wawaelimishe namna ya kupata haki ya kumiliki vitalu " Alisema Kamonga.                                   

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya amesema hoja hizo ni za msingi huku akiahidi kutoa ushirikiano kwenye uwezekano kwa wabunge hao ili kufikisha hoja na bungeni na kutetea maeneo yaliyoshikiliwa kwa muda mrefu bila kutumika.

Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akieleza kusikitishwa na vitalu vingi kushikiliwa  katika jimbo lake bila kutumika huku akiomba serikali kuona namna ya kusitisha leseni za vitalu visivyotumika.
Baadhi ya wajumbe katika kikao cha ushauri mkoa wa Njombe wakiwa makini kusikiliza hoja za kuendelea kukuza uchumi wa mkoa wa mko wa uchumi wa Njombe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...