MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amesema ni wajibu wa kila mkazi wa jiji hilo kuhakikisha anasafisha mazingira ambapo ameeleza kuwa Mkoa umeandaa mipango kabambe ya kufanya jiji kuwa katika hali ya usafi na kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.
RC Kunenge amesema miongoni mwa mikakati hiyo ni pamoja na kuitumia Kampuni ya usafi ya JKT kufanya usafi kwenye baadhi ya maeneo ya jiji hilo ambapo pia amezielekeza Manispaa za jiji hilo kuongeza adhabu kwa wanaotapisha maji taka kwenye makazi na mitaro ya maji ya mvua.
Aidha RC Kunenge amesema mikakati mingine ni uboreshaji wa madampo ya taka, Ujenzi wa Kiwanda cha kuchakata taka na kugeuza kuwa mbolea, upandaji wa Miti, utunzaji wa bustani na kushirikiana na wadau wakiwemo benki ya ya CRDB kupanda miti na Shirika la Sigara ambalo litatoa mapipa 50 kila mwezi ya kuhifadhi taka.
Hata hivyo RC Kunenge amesema Serikali imedhamiria kupatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi ikiwemo ujenzi wa miundombinu, unoreshaji wa huduma za Afya, Elimu, Maji na kuweka mazingira Bora ya biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...