Mitandao ya kijamii ya Facebook, na Twitter imesitisha kurasa za Rais wa Marekani Donald Trump, kufuatia hatua ya wafuasi wake kuvamia bunge la Marekani.Mtandao wa Twitter umemfungia Trump ukurasa wake asiweze kuutumia kwa muda wa saa 12, na kuonya kwamba utaufunga kabisa ukurasa huo endapo Trump ataendelea na ukiukaji wa kanuni.

Kampuni hiyo ya mawasiliano pia iliilazimu timu ya Trump kufuta jumbe tatu ikiwemo video fupi ambayo Trump aliwahimiza wafuasi wake kwenda nyumbani lakini akirudia madai yake kuwa uchaguzi ulikumbwa na udanganyifu.Majukwaa ya Facebook na Instagram pia yalitangaza kwamba Trump hataweza kutumia kurasa zake kwa muda was aa 24 zijazo kufuatia ukiukaji wa sera zake.Ikulu ya Marekani haikutoa jibu la moja kwa moja kufuatia hatua za mitandao hiyo ya kijamii.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...