Mabaraza ya bunge la Marekani yamemthibitisha rais mteule Joe Biden kuwa mshindi wa rais katika uchaguzi uliofanyika Novemba.Mabaraza hayo mawili yalitupilia mbali matakwa ya wapambe wa Trump kwamba matokeo katika majimbo ya Arizona na Pennsylvania yabatilishwe.
Baada ya kukamilika kwa mchakato huo, seneta Amy Klobuchar alisema wameweka rekodi kwamba Biden atakuwa rais na Harris makamu wake kulingana na kura ambazo wamepewa.Punde baada ya ushindi wa Biden kuidhinishwa, Rais Trump ametoa taarifa akiahidi makabidhiano ya amani ya madaraka huku akidokeza kuwa atasalia kwenye siasa, hatua inayoibua gumzo kwamba atataka kuwania tena urais mwaka 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...