Na Miza Kona / Maelezo Zanzibar 

RAIS Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar awamu ya saba Dk. Ali Mohamed Shein amesema Mapinduzi ya mwaka 1964 yamekuja kumkomboa mnyonge kutoka katika ubaguzi na kuweza kujitawala .  

Dk. Shein ameyasema hayo huko Uroa Wilaya ya Kati Unguja wakati wa ufunguzi wa kituo cha Ubunufu wa Kisayansi kwa niaba ya vituo 21 vilivyojengwa ikiwa ni shamra shamra ya maadhimisho ya kutimiza miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema Mapinduzi yameleta umoja, mashirikiano, mshikamano, maridhiano na mapenzi kwa wazanzibari na kuweza kjitawala wenyewe na kupata huduma zote muhimu za kijamii ikiwemo elimu ambayo ni mkombozi wa maendeleo.

“Mapinduzi yameleta mambo muhimu ya msingi ikiwemo elimu na afya ambapo hapo awali ilikuwa ikitolewa kwa ubaguzi na wananchi waliowanyonge hawakupata fursa hiyo kwani nafasi hizo walinufaika mabepari”, alieleza Dk Shein.

Dk. Shein ameeleza elimu ya sayansi ni kichocheo kikubwa cha kuleta maendeleo nchini hivyo amewata wazazi na walimu kuwashajihisha wanafunzi kujikita kusoma masomo ya sayansi ili kukuza kiwango cha elimu kwa kuleta maendeleo na kupata wataalamu wazuri.

Amefahamisha kuwa nchi nyingi duniani zimekuwa zikiwasomesha vijana wake masomo ya sayansi ili kuboresha elimu na kupata vijana wenye taaluma mbali mbali nchini kwa lengo kupata ufanisi zaidi.

Dk. Shein amesisitiza kuvitumia na kuvitunza vituo hivyo ili viweze kudumu na kuweza kupata wataalamu na kuongeza ufanisi kwa vjiana katika masomo ya sayansi.

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Simai Mohamed Said amesema vituo hivyo vitawasaidia vijana kutumia ubunufu wao na ujuzi waliokuwa nao katika kujifunza zaidi na kuweza kujipatia ajira kupitia utaalamu walionao.

Akitoa taarifa ya kitaalamu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dk. Idrisa Muslim Hija amesema mradi huo una lengo la kuimarisha ubora wa elimu katika masomo ya sayansi na Hisabati kwa ngazi elimu ya sekondari na kiingereza kwa elimu ya msingi.

Aidha amefahamisha kuwa pia utainua ubora wa elimu Zanzibar hasa katika kuongeza ufaulu kwa wanafunzi na kuimarisha usomeshaji katika masomo ya sayansi, hisabati na lugha ya kiingereza.

Mradi huo wa miaka mitano 5 umejengwa kupitia mradi wa Zanzibar Improving Student (ZIPS) ambao umefadhiliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mkopo wa Benk ya Dunia na umegharimu Dola za Kimarekani milioni 35 hadi kumalizika kwake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...