Na Ramadhani Ali - Maelezo   

WAJASIRIAMALI wa Zanzibar wamezishauri Taasisi zinazosimamia usalama
wa Chakula na Vipodozi ambazo sio za Muungano kuzitafutia ufumbuzi
changamoto zinazowakabili wanaposafirisha bidhaa zao Tanzania Bara.

Wameeleza kilio chao wakati Viongozi wa Wakala wa Chakula na Dawa
Zanzibar (ZFDA) walipokutana na Wajasiriamali hao katika Ukumbi wa
Mama na Mtoto Kidongochekundu kuwaeleza mchakato wa kuingia
makubaliano na Taasisi ya Viwango Tanzania (TBS) ili kuwarahisishia
shughuli zao.

Katibu wa Jumuiya ya ya Wasafirishaji bidhaa nchi za nje Khamis Issa
amelalamika vitambulisho vya kusafirishia bidhaa vinavyotolewa na
Taasisi zinazosimamia usalama wa Chakula  Zanzibar, ZBS na ZFDA
havitambuliki Tanzania Bara kwa madai kuwa sio Taasisi za Muungano.

Amezishauri Taasisi za Tanzania Bara na Zanzibar zinazoshughulikia
usalama wa bidhaa kukaa pamoja, kushirikiana na kuaminiana katika
kujenga umoja na ushirikiano wa pande mbili za Muungano.

Mjasiriamali kutoka Jumuiya ya Wafanyabiashara Wanawake Zanzibar
(ZWCC) Zeyana Ahmed Kassim amesema TBS imeandaa mazingira ya
kuwasaidia Wajasiriamali wa Tanzania Bara lakini mpango huo haupo kwa
Zanzibar.

Amesema hali hiyo hupelekea baadhi ya wajasiriamali kutoka Zanzibar
kuomba kujiunga na Shirika la Viwango Tanzania Bara ili kuepukana na
usumbufu wakati wanaposafirisha bidhaa zao.

Amekumbusha kuwa tokea kuingia madarakani Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amekuwa
akisisitiza nia yake ya kusaidi sekta binafsi wakiwemo Wajasiriamali
dhana ambayo inahitaji kuungwa mkono na wadau wote.

Awali akizungumza na Wajasiriamali hao, Mkurugenzi Idara ya Dawa na
Vipodozi wa ZFDA, Bora Lichanda aliwaeleza wajasiriamali walioshiriki
mkutano huo kwamba lengo lao ni kuwaondoshea vikwazo wanavyokabiliana
navyo katika kutekeleza shughuli zao

Ameahidi kuwa mapendekezo waliotowa kwenye kikao hicho
watayawasilisha kwa wenzao wa Tanzania Bara kabla ya mchakato wa
kuingia makubaliano na TBS haujakamilika.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...