Mbunge wa Makete ameshirikiana na Wananchi wa Mang'oto vijiji vyote kufanya kazi ya maendeleo kwa kusafisha Intake ya Maji iliyopo kwenye milima umbali wa KM 7 hadi 8 kutokea kijiji cha Malembuli.

Ni masaa 2 yametumika kupanda mlima huo na baadae kufika eneo lililotegwa Maji ambalo takribani wiki nzima limeziba na kusababisha ukosekanifu wa Maji kwa Wananchi wa Mang'oto.

Sanga ambaye ameshirikiana na wananchi hao kusafisha intake amesema " nawashukuru wananchi kwa kujitokeza kwa wingi, nimepanda mlima huu kwa tabuu kweli na sehemu zingine ilinibidi niweke vituo vya kupumzika hadi nimefika, Furaha yangu ni kujumuika nanyi kwenye kazi hii ambayo kwa leo imeleta matumaini ya kupatikana kwa Maji, nawashukuru kwa uchaguzi, mmetuamini tushirikiane kwenye kuchapa kazi"

Sanga anafika Mang'oto kwa mara pili ndani ya wiki moja ambapo siku chache zilizopita alikwenda kijiji  cha Ilindiwe kufunga Solar ya Umeme kwenye Zahanati ili huduma za Afya zitolewe wakati wote usiku na mchana.




 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...