HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani katika kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha usafi wa mazingira na kuthibiti kutokea kwa amlipuko wa magonjwa mbali mbali imeamua kuweka sheria ndogondogo zitakazotumia kuwachukulia hatua kali wananchi watakaobainika kutupa uchafu ovyo ambao unaweza kuhatarisha usalama wa afya zao ikiwemo kuwapiga faini ya kuanzia kiasi cha shilingi laki mbili na kuendelea.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya
ya Kisarawe Mussa Gama wakati akizungumzia kuhusiana na mikakati
endelevu waliyoiweka katika kutekeleza azma ya agizo la Makamu wa
Rais la Mama Samia Suluhu la wananchi wote kufanya usafi katika kila
jumamosi ya mwisho wa mwezi na kwamba itaweza kuwasaidia wananchi
kuondokana na ile hali ya kupata magonjwa ya mlipuko.
Gama alibainisha kwamba lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanaweka
misingi imara kwa ajili ya kuboresha usafi wa mazingira katika maeneo
mbali mbai ikiwemo katika masoko, zahanati, hospitali pamoja na sehemu
za barabarani.
“sisi kama halmashauri ya Kisarawe hatuna mzaha kabisa katika suala
zima la usafi wa mazingira nah ii ni hatua ya utekelezaji wa maagizo
ambayo yalitolewa na Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu ya kuhakikisha
kwamba wananchi wote wanafanya usafi katika maeneo yao ya makazi nay
ale ya biashara katika kila juma mosi ya mwisho wa mwezi na sisi ili
tunalifanya kazi ipasavyo bila masihala,”alisema Gama.
Aidha Gama katika kutimiza azma hiyo ya serikali ya awamu ya tano
katika kuwathibiti baaaadhi ya watu ambao wamekuwa wakienda kinyume
cha sheria na taratibu ambazo zimewekwa tayari wameshaweka sheria kali
kwa kushirikiana na baraza la madiwani ambazo zitatumika katika
kuwawajibisha wale wote ambao watabainika wanachafua mazingira kwa
makusudi.
Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa kwa sasa katika halmashauri ya Wilaya
ya Kisarawewananchi walio wengine tayari wameshaanza kuyazingatia
maelekezo mbali mbali ambayo yanatolewa na wataalamu wa afya kuhusiana
na madhara ya utupaji wa taka ovyo yanaweza kusababisha kutokea kwa
milipuko ya magonjwa mbali mbali.
Katika hatua nyingine Gama hakusita kuwaasa wananchi wote wa
halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kuhakikisha kwamba wanaendelea
kuzingatia misingi ya kulinda afya zao kwa kuendelea kunawa mikono yao
kwa kutumia maji tiririka na sabuni wakati wa kula vyakula kwa lengo
la kuthibiti hali ya kutokea kwa magonjwa ya aina mabli mbali kama
vile kuhara pamoja na kuumwa na matumbo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...