MFANYABIASHARA
Sadikiel Meta, 71 aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka 41 yakiwemo ya
kuwatumikisha walemavu na kuwafanya kuwa omba omba amefariki dunia.
Taarifa
hiyo imetolewa leo Februari 9,2021 na wakili anayemtetea mshtakiwa huyo
Robert Langeni baada ya kesi hiyo kuitwa mahakamani hapo kwa ajili ya
kutajwa
"Mteja wangu amefariki tangu Januari 28 mwaka huu katika Hospitali ya Temeke alipokuwa amelazwa", amesema wakili Langeni.
Mapema wakili wa serikali Kija luzungana alidai mbele ya Hakimu Mkuu Mkazi
,
Kassian Matembele wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa kesi hiyo
ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini hana jalada la uchunguzi la kesi
Hata
hivyo mahakama haikusema lolote juu ya taarifa hiyo ya kifo kutoka kwa
wakili wa mshtakiwa na ikiahirisha kesi hadi Februari 23, 2021
itakapokuja tena kwa ajili ya kutajwa
Katika kesi hiyo Meta
anashtakiwa na wenzake 14 ambapo mbali na shtaka la kuwatumikisha
walemavu na kuwafanya kuwa omba omba mashtaka mengine ni usafirishaji
haramu wa binadamu, kutakatisha fedha, kukwepa kulipa kodi na ba
kuisababishia serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hasara ya
zaidi ya sh. Milioni 31.3
Mbali na Meta baadhi ya washtakiwa
wengine katika kesi hiyo ni, Yusuph Mohamed (35), Yusuph Magadu (20),
Emmanuel Salu (20) Gogad Mayenga (18), Samson Taruse (26), Hussein John
(18), Zacharia Paul (18), Dotto Shigula (19), Petro Simon (21), Emmanuel
Sahani (38), Joseph Mathias (20), Masanja Paul (21), Aminiel Sangu
(19), na Emmanuel Lusinge.
Wanadaiwa kati ya mwaka 2020 na
Januari Mosi 2021 jijini Dar es Salaam, kwa pamoja walishiriki kufanya
uhalifu wa kupanga kwa kuongoza genge la uhalifu na kutekeleza
kufanikisha kusafirisha binadamu kwa haramu.
Pia katika shtaka la
usafirishaji haramu wa binadamu inadaiwa, katika kipindi hicho hicho
huko Tandale ndani ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam mshtakiwa
Meta na Mohamed waliwatumikisha walemavu 37 na kuwafanya wawe omba omba
wa mtaani kwa lengo la kujipatia kipato.
Miongoni mwa wa
walemavu hao ni mtoto Kashinje Emmanuel, mwenye umri wa miaka saba,
Doto Silas Happines Bezagurwa, Neema Edward na Peter Sereke wote wa ama
umri wa miaka 11.
Imedaiwa wa washtakiwa hao pia walikuwa
wakisafirisha walemavu kutoka mikoa ya Shinyanga na Tabora kwenda Dar es
Salaam na kwamba wakishapokelewa wanawaingiza kwenye shughuli za omba
omba kwa lengo la kujipatia faida.
Aidha mshtakiwa Meta anadaiwa kushindwa kulipa kodi ya thamani ya Sh. 31,328,500.31 kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) .
Pia mshtakiwa Meta anadaiwa kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya Sh. Milioni 31.3.
Katika
shtaka la mwisho la utakatishaji imedaiwa kati ya Agosti 2020 na
Januari Mosi 2021, mshtakiwa Meta alijipatia Sh. Milioni 31,328,500.31
huku akijua kuwa fedha hizo ni zao la kosa tangulizi la kushindwa kulipa
kodi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...