NA  YEREMIAS  NGERANGERA….NAMTUMBO.

Baraza la wafanyakazi  katika  Halmashauri ya wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma  limepitisha mapendekezo  ya  bajeti  ya Halmashauri  kwa mwaka wa fedha  2021/2022 ikikisiwa kukusanya  na kupokea jumla  ya Tsh .28,337,660,400 kutoka  vyanzo vya ndani,ruzuku kutoka serikali kuu na michango kutoka kwa wadau wa maendeleo.

Akisoma bajeti hiyo afisa  mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo  bwana  Amos  Kanige  alisema  Halmashauri  inakisia kukusanya  kiasi cha Tsh 1,588,000,000 kutoka mapato ya ndani  na inakisia kupokea  Tsh 22,871,067,500 kutoka serikali kuu na Tsh.3,778,592,900 kama ruzuku  kutoka kwa wahisani.

Kanige  alifafanua  matumizi ya bajeti hiyo  kuwa  Tsh  18,043,444,000 itatumika  katika mishahara ,Tsh 2,858,693,000 kwa ajili  matumizi  mengineyo  na Tsh 7,337,660,400 kwa ajili  ya matumizi  ya miradi ya maendeleo.

Hata hivyo bwana  Kanige alisema katika mpango wa mapendekezo  ya bajeti  kwa mwaka 2021/2022 Halmashauri  imezingatia  sheria, kanuni,  taratibu na miongozo  iliyowekwa  na serikali katika kuandaa bajeti  hiyo na ushirikishwaji  wa wananchi  katika kutekeleza  miradi  mbalimbali ya maendeleo.

Kupitia bajeti  hiyo  Kanige alisema kutakuwa na  uboreshaji   wa huduma za elimu kuanzia elimu ya awali hadi kidato cha sita, uboeshaji wa huduma za afya  kwa kuimarisha huduma za tiba na kinga ,kuimarisha vyanzo vya mapato ya ndani kwa kununua mashine 10 ya kukusanyia mapato,kuboresha stendi ya mabasi Namtumbo,kununua  na kusambaza  mbegu ya ufuta  na kuendeleza ujenzi wa soko la kisasa Namtumbo.

Aidha katika bajeti hiyo hiyo kutakuwa na uimarishaji wa huduma za kilimo na mifugo kwa kutoa huduma za ugani katika kata 21,ukarabati wa skimu za umwagiliaji na kujenga skimu 2 mpya ,ukarabati  wa machinjio moja,kufanya mpango wa matumizi bora ya ardhi , kuanzisha mnada wa mifugo pamoja na utoaji wa mikopo kwa vikundi 65 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu  ikiambatana  na utoaji wa ruzuku  ya fedha  kwa kaya  4637 katika vijiji 42.

Katibu wa chama cha walimu wilayani  Namtumbo Mtamila Achikuo  pamoja na kupongeza mapendekezo ya bajeti  alidai amefurahishwa na kuingizwa katika bajeti  kikao cha baraza la wafanyakazi  tofauti  na bajeti  zilizopita ambazo zilisababisha malalamiko ya wajumbe wa kikao kutolipwa stahiki zao kwa wakati walipokuwa wakihudhuria vikao vya baraza la wafanyakazi  ambalo lipo kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa Mwekahazina  wa Halmashauri ya wilaya Namtumbo  Pendo  Nyomeye  alisema mpaka kufika  juni 30,2020 mapato halisi yaliyokusanywa  ni Tsh 22,302,818,436.19 sawa na asilimia 91.79 ya fedha  iliyoidhinishwa  huku makusanyo ya mapato ya ndani yalikuwa 1,694,578,977.53 sawa na asilimia 119.6 ya lengo la mwaka ,mishahara  Tsh 16,434,760,623,23.matumizi mengineyo Tsh 1,313,064,100 na Tsh 2,860,414,735.40. kwa ajili ya maendeleo.



Afisa mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo Amos Kanige aliyesimama  akiwasilisha mapendekezo ya bajeti ya Halmashauri kwa mwaka 2021/2022

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...