Ubalozi wa Tanzania mjini muscat Oman umefungua maombolezi ya kifo cha Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Marehemu Maalim Seif Sharif Hamad. Maombolezi hayo yalifanyika kwa muda wa siku mbili huko nyumbani kwake Mh.Balozi Abdallah Kilima na viongozi na mabalozi wa nchi mbali mbali kuhudhuria kwenye maombolezi hayo.
Bw. Ahmed Ali Amri akisaini katika kitabu cha maombolezoBw. Ahmed Ali Amri akiwa na balozi wa Tanzania nchini Oman Mh. Abdallah Kilima baada ya kusaini katika kitabu cha maombolezo
Bw. Sayyid Mohamed Salim Al Said kutoka kwenye familia ya Ufalme wa Oman akisaini kitabu cha Maombolezo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...