

……………………………………………………………………………..
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MKUU wa wilaya ya
Kibaha ,mkoani Pwani ,mhandisi Martin Ntemo, ametoa siku mbili kwa
wafanyabiashara ndogondogo wa Soko la Picha ya Ndege ,kuondoka katika
eneo la hifadhi ya barabara ili kumpisha mkandarasi aendelee na ujenzi
wa barabara kuu .
Akizungumza na
wafanyabiashara hao a,katika soko hilo ,alieleza amesikia malalamiko
kuwa kuna baadhi ya wafanyabishara wanadaiwa kuchochea kuwashinikiza
wafanyabiashara wengine wasihame katika eneo lililotengwa.
Ntemo alisema
wafanyabiashara walitakiwa kuhamia , eneo la shirika la elimu ambalo
lipo river road Msufini lakini walikaidi na kudai kuwa hakuna huduma
muhimu kama vile umeme, na sio eneo la kudumu.
“Hili eneo ni
hatarishi na Tanroad walishawaelekeza wahame ili mkandarasi aendelee na
ujenzi , ikanisukuma nikaenda kuzungumza na taasisi ya shirika la elimu
wakaruhusiwa waendele na biashara zao lakini nikabaini kuna
wafanyabiashara wachochezi wanaoshawishi wenzao Wagome kuhamia katika
eneo hilo”
Msimamizi wa mradi huo kutoka TANROADS
Charles Rwetabura,
alifafanua wafanyabishara hao wanapaswa kuondoka kwenye eneo la mradi wa
kuboresha maeneo hatarishi kwa malengo mawili ikiwemo
Sheria ya barabara
namba 13 ya mwaka 2007, inayowataka wananchi waliovamia maeneo hatarishi
waondoke , lakini pia suala la usalama.
Diwani wa kata Sofu
,Musa Ndomba alisisitiza wajasiriamali hao , kutii agizo hilo na kuhama
ambapo kwasasa itakuwa eneo la kudumu ili kuleta maendeleo na kuinua
uchumi wa kata hiyo.
Awali mmoja wa
wafanyabishara hao ,Daniel Singa alibainisha mgogoro huo ni wa takriban
miaka sita ambapo mwanzo walitakiwa kuhamia eneo la Lulanzi ambako
waliona ni mbali , baadae wakatakiwa kuhamia eneo la River road ambako
wachache waligomea .
Singa alielezea kwamba ,kwa sasa wametii agizo la serikali na wataondoka kwa ajili ya maendeleo yao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...