Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

NI Patashika Nguo kuchanika katika Michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup msimu wa 2020-2021 baada ya kufika hatua ya 32 Bora.

Droo ya Michuano hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam ambapo Mabingwa Watetezi wa Michuano hiyo, Simba SC wamepangwa kucheza na African Lyon ya Dar es Salaam wakati watani wao, Yanga SC wakipangwa na Kengold FC ya jijini Mbeya.

Timu nyingine za Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ni Dodoma Jiji FC ambao watacheza na Kipigwe FC, Polisi Tanzania dhidi ya Kwamndolwa FC, Azam FC dhidi ya Mbuni FC, Tanzania Prisons wao watacheza dhidi ya Sahare All Stars na Biashara United ya Mara dhidi ya Trans Camp.

Wengine ni KMC FC ya Kinondoni dhidi ya Kurugenzi FC, Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani dhidi ya Mbao FC, Kagera Sugar dhidi ya Eagle Stars, Coastal Union wao watacheza dhidi ya Ihefu FC na Mwadui FC wakiumana na Gwambina FC.

Mtibwa Sugar dhidi ya JKT Tanzania, Namungo FC watakuwa na kibarua dhidi ya Mbeya City, Arusha FC dhidi ya Mashujaa, Tunduru Korosho dhidi ya Rhino Rangers.

Michezo yote itaanza kuchezwa Februari 27 na 28, 2021 katika Viwanja mbalimbali hapa nchini.

Michezo ya Nusu Fainali ya Michuano hiyo itachezwa katika viwanja viwili ambavyo ni Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora kwa Nusu Fainali ya kwanza na Nusu Fainali ya Pili itachezwa Uwanja wa Majimaji, Songea na Fainali itachezwa Uwanja wa Lake Tanganyika Kigo
ma.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...