Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) Prof.Lazaro Busagala amewaomba wananchi wa mkoa wa Arusha na mikoa ya jirani kutembelea katika banda la Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC) kwa ajili ya kupata elimu ya teknolojia ya nyuklia na udhibiti wa matumizi salama ya mionzi nchini.
Amesema hayo kwenye maonesho ya nne ya mfuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea Jijini Arusha ambapo amesema wananchi watapata uelewa juu masuala mbali mbali kuhusiana na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania(TAEC).
‘ Tuna watalaamu mbali mbali hapa katika maonesho ambao wataweza kuwapa uelewa wananchi kwa ujumla hivyo nawaomba wafike kwa wingi kujionea namna tunavyofanya kazi”alisema Prof. Busagala.
Pia Prof Busagala amekagua shughuli za TAEC kwenye maonesho hayo, ambayo yemefunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Kassim Majaliwa.
Home
HABARI
WANANCHI ARUSHA WAOMBWA KUTEMBELEA BANDA LA TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI TANZANIA (TAEC) KUPATA ELIMU TEKNOLOJIA YA NYUKLIA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...