Na.Vero Ignatus
Elimu ya ujasiriamali iliyotolewa katika wilayani Ngorongoro,kwa wanawake na vijana kutoka vikundi vinne imesaidia kuondokana na hali ya utegemezi ,ambapo wameweza kuuanzisha vikundi vya kuweka na kukopa ,na vimewasaidia kuuanzisha miradi ya kiuchumi
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea vikundi hivyo ambavyo ni Nosotwa na New Vision and Development,wanufaika hao wamesema awali kabla ya kuanzisha vikundi na miradi hiyo hali zao kiuchumi hazikuwa nzuri.
Aidha kabla ya kuanzishwa kwa vikundi hivyo mapema mwaka jana,mwaka 2015 baadhi ya wanavikundi hao walikabidhiwa ng’ombe ili kuondokana na hali ngumu ya kimaisha inayowakabili,ambayo ilitolewa na Shirika la Oxfam,kupitia wadau wake,Shirika la PALISEP.
Mmoja wa wanaufaika hao kutoka kijiji cha Enguserosambu,Naiseku Shimbo,alisema kupitia vikundi hivyo vilivyoanzishwa mapema mwaka jana,vimewawezesha kuanzisha miradi mbalimbali ya vikundi pamoja na miradi binafsi hali inayochangia kuondokana na utegemezi.
Pichani ni Mmoja wa wanaufaika hao kutoka kijiji cha Enguserosambu,Naiseku Shimbo,alisema kupitia vikundi hivyo vilivyoanzishwa mwaka jana,ameweza kuuanzisha biashara kuuza vinywaji,chakula,mazao pamoja na kununua mifugo na kuwa hadi sasa ana ng’ombe 10 na kondoo 100.
Alisema mwaka 2015 alipewa ng’ombe mmoja na kuanza biashara ya mamalishe,ambapo hadi sasa zimemuwezesha kuwa na biashara nyingine ikiwemo ya kuuza vinywaji,chakula,mazao pamoja na kununua mifugo na kuwa hadi sasa ana ng’ombe 10 na kondoo 100.
“Nashukuru sana PALISEP kwani kabla ya kunipa ngo’ombe nilikuwa masikini,nadhaulika baada ya kupata ng’ombe nilijisikia vizuri watoto walipata maziwa,nikauza mengine nikapata chakula cha nyumbani maisha yakabadilika,”alisema
Kuhusu vikundi alisema PALISEP waliwafundisha juu ya elimu ya ujasiriamali iliyoweza kuwasaidia kutambua namna ya kufanya biashara,kuanzisha kikundi ambacho kimewasaidia kujiwekea fedha.
Baada ya mafunzo na kuelewa namna ya kutunza fedha,mwaka jana tulianzisha kikundi ambacho kina wanachama 15 ambacho mwaka huu tumevunja na kupata Sh Milioni tano ambazo tumetumia kununua kondoo 20 wa kufuga na mwezi wa nane tutauza na hela itaongezeka.
Alisema elimu hiyo ya ujasiriamali imewasaidia kufahamu namna ya kutafuta maendeleo,huku kuhusu unyanyasaji wa wanawake katika jamii hiyo ukipungua ambapo wanaume wengi wameruhusu wake zao kufanya biashara mbalimbali.
Meneja wa Miradi, Oxfam, kanda ya kaskazini,Donath Fungu,alisema mradi huu unafadhiliwa na shirika la Oxfam Hongkong na unatekelezwa katika wilaya mbili za Ngorongoro na Hanan'g ya mkoani Manyara.
Alisema lngo kuu ni kuwainua wanawake na vijana kiuchumi na na kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi kupitia shughuli mbali mbali za kiuchumi kama vile kilimo endelevu cha alizeti na mboga mboga kupitia vitalu nyumba, na shughuli nyingine za kiuchumi kama asali na uchimbaji chumvi.
Alisema kupitia shughuli hizo huwasadia wanawake na vijana kukabiliana na janga la mabadiliko ya tabia nchi ambayo huathiri shughuli za kilimo ambacho ndiyo chanzo kikuu cha mapato kwa jamii tunayoihudumia
"Sambamba na hilo pia tumejikita na na kupambana na utatua migogoro ya ardhi hususan kwa wanawake wajane kwa kuwapatia hati miliki za kimila, mradi unaamin kwa kufanya hivyo kutamwezesha mwanamke kuwa salama, kuweza kumiliki rasilimali na kumwongezea kipato kwa kufanya shughuli zake za kilimo endelevu, ili kuongeza thamani ya ardhi,"alisema
Naye Baraka Laizer kutoka kikundi cha New Vision and Development,kilichopo kata ya Lopolu,alisema katika kikundi hicho chenye wanawake 28 na vijana wawili,wameweza kuanzisha kilimo cha mbogamboga kupitia kitalu nyumba.
Anasema baada ya mafunzo ya PALISEP wameweza kuanzisha kilimo hicho mwaka jana ambapo walilima nyanya,hoho na matango na kuweza kupata Sh milioni 1.5 katika msimu huo ambazo wanatarajia kutumia kama mtaji katika msimu wa mwaka huu wa kilimo hicho.
“Kiukweli tumeona faida za kitalu nyumba tofauti na mfumo wa kawaida wa kilimo ikiwemo mazao kuwa na hali nzuri,hayajashambuliwa na wadudu hivyo ilitusaidia sana sokoni bidhaa zilinunuliwa kwa haraka,”alisema
Naye Kerisho Kitupei,kutoka kikundi hicho alisema elimu hiyo ya ujasiriamali imesaidia kuinua jamii ya kimasai hasa wanawake na vijana na kupitia mradi huo wanakikundi hao wameweza kuanzisha biashara zao nyingine.
“Kuna baadhi ya wanakikundi walikuwa hawana shughuli,ila baada ya kupewa elimu wameanzisha biashara na tumeona mafanikio makubwa sana,tunashukuru wadau kwa msaada huu,”
Kwa upande wake Afisa Kilimo kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,Laurance Ledio,aliwapongeza wadau hao kwa kutoa elimu juu ya namna ya kuweza kufanya kilimo chenye tija na kuzalisha mazao kwa kufuata kanuni.
“PALISEP na Oxfam ni wadau wetu na tumekuwa tukishirikiana nao ila katika hili la kuanzisha vitalu nyumba viwili katika halmashauri hii ambavyo awali havikuwepo na matumizi ya teknolojia ya kitalu nyumba na umwagiliaji kwa njia ya matone,itasaidia sana kukuza kilimo,”
Alisema faida za teknolojia hizo ukilinganisha na kilimo cha kawaida ni pamoja na kusaidia kupunguza wadudu kushambulia mazao na kuepuka magonjwa mbalimbali.
Akizungumzia namna jamii ilivyopokea teknolojia hiyo,alisema awali wananchi walikuwa wakishangaa ila baada ya elimu zaidi kutolewa wengine wameanzisha kilimo cha umwagiliaji wa matone katika maeneo yao.
“Tunatakiwa kuungana na wadau wengine katika kusaidia jamii hata mafunzo namna gani wanaweza kufanya uzalishaji kupitia kitalu nyumba kufundisha vijana ili tuwe na mafundi ambao wataelimisha na wenzao,”

Katika Picha ni Afisa Kilimo kutoka halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro,Laurance Ledo
,aliwapongeza wadau hao kwa kutoa elimu juu ya namna ya kuweza kufanya kilimo chenye tija na kuzalisha mazao kwa kufuata kanuni.
Naye Kaimu Afisa Maendeleo ya jamii kutoka halmashauri hiyo,Thomas Nade,alisema wadau wa maendeleo ni mkono wa pili wa serikali na kuwa pale inapokuwa imeshindwa kudika wadau wa maendeleo wanafika na kusaidia miradi mbalimbali.
Aidha aliwapongeza wadau hao kwa kuwasaidia uwezeshaji wanawake na vijana na kuwa wamekuwa wakisaidia kupiga vita suala la ukandamizaji wa wanawake.
“Namna pekee ya kumwezesha mwanamke kiuchumi ni pamoja na kuhakikisha tunatumia wazee wa mila na wadau wengine kupinga mila zinazokandamiza kundi hilo na ukiangalia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kwani awali haikuwa rahisi mwanamke kujishughulisha na biashara au kwenda kwenye Vicoba,”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...