NA TIGANYA VINCENT,RS TABORA
MLENGWA wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) Wilayani
Igunga Mkoani Tabora Vivian Makala amefanikiwa kujenga nyumba ya
kuishi, kusomesha watoto baada ya kupata fedha za ruzuku ya TASAF na
kuanzisha mradi wa kuuza mchele.
Mlengwa huyo alitoa ushuhuda huo jana wakati ziara ya mfunzo ya viongozi wa Mfuko wa
Maendeleo ya Jamii (TASAF) na waandishi wa habari walipokuwa kujifunza mafanikio ya walengwa yaliyotokana na fedha hizo.
Makala
alisema baada ya kupata fedha za TASAF alianza kwa kukunua gunia mmoja
ya mpunga na kulikoboa ambapo alipata kilo 60 alizoziuza kwa shilingi
1,800 kwa kilo na kupata 108,000/= ambazo zilimwezesha kupata mtaji wa
kuboresha biashara ya uuzaji mpunga.
Alisema
hatua hiyo ilimfanya kutumia fedha hizo kumkopesha mkulima wa mpunga
aliyezitumia kulimisha katika mbuga yake na kuzirejesha kwa kumpa gunia
23 baada ya kuvuna na ndipo hapo mtaji wake uliongezeka.
Makala
alisema kutokana fedha anazopata kutokana na mauzo ya mchele
amefanikiwa kununua eneo na kujenga nyumba ambayo ndio anaishi.
Alisema
faiada nyingine aliyoipata ni pamoja na kusomesha watoto wake kwa
kuwapa mahitaji muhimu kama vile sare, viatu na maftari na kuwa na
uhakika wa watoto wake kula milo mitatu kwa siku.
Makala
aliongeza kuwa fedha anazopata kutokana na mauzo ya mchele zimekuwa pia
zikimsaidia katika matibabu yake ya ugonjwa wa miguu ambao umekuwa
ukimsumbua kwa muda mrefu na kumfanya asiwe na uwezo wa kusimama kwa
muda mrefu.
Alisema
tatizo hilo limemfanya kushindwa kujishughulisha na shughuli za
shambani na hivyo kupata mtaji huo kumemsaidia kuweza kupata mahitaji
yake ya kila siku.
Mlengwa huyo alisema ni vema kwa walengwa wanapata ruzuku kupitia mpango huo kutumia fedha wanazopewa katika shughuli za uzalishaji mali kwa lengo la kujiua kiuchumi na kuachana na umasikini na wasirudi nyuma .
Mlengwa huyo alisema hata akitolewa katika Mpango huo hawezi kushindwa kujimudu yeye na familia yake katika m mahitaji mbalimbali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...