Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi zawadi
ya ngao mfanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika
nafasi ya kwanza Mtoka David Mtoka wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza
wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo
pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni mbili.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti mfanyakazi bora wa robo
ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika nafasi ya pili Mohamed Songoro
wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo
katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi
milioni moja na laki tano
Mkurugenzi wa Kurugenzi
ya Utawala na Fedha wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) CPA Agnes Kuhenga
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Kurugenzi hiyo pamoja
na wafanyakazi wa kitengo cha Ununuzi na Ugavi mara baada ya kumalizika kwa
hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora wa robo ya pili ya mwaka wa fedha wa
2020/2021. Wapili kushoto ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya kwanza Mtoka David
Mtoka aliyetoka katika kurugenzi ya Utawala na Fedha, wapili kulia ni
mfanyakazi aliyeshika nafasi ya pili Mohamed Songoro aliyetoka katika kurugenzi
ya Utawala na Fedha na katikati ni mfanyakazi aliyeshika nafasi ya tatu Lucas
Jilulu aliyetoka katika kitengo cha Ununuzi na Ugavi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya
Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimkabidhi cheti mfanyakazi bora wa robo
ya pili ya mwaka wa fedha 2020/2021 aliyeshika nafasi ya pili Mohamed Songoro
wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza wafanyakazi bora watatu iliyofanyika leo
katika Taasisi hiyo. Mfanyakazi huyo pia alipewa zawadi ya fedha taslimu shilingi
milioni moja na laki tano.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...