Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akizungumza na Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
mkoani humo Bi. Eunice Liheluka na Afisa Kodi Mkuu wa TRA Makao Makuu Bw. James
Ntalika wakati walipomtembelea ofisini kwake kuzungumzia kampeni ya elimu kwa mlipakodi
inayoendelea jijini humo.

Meneja wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya Bi. Eunice Liheluka akizungumza na timu ya
maafisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kutoka Makao Makuu (hawapo pichani) wakati
walipomtembelea ofisini kwake kwa ajili ya kupanga mikakati ya kutekeleza
kampeni ya elimu kwa mlipakodi mkoani humo.
Afisa Kodi Mkuu wa Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) Bw. James Ntalika akiwaelimisha wanunuzi wadogo wa madini
Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya wakati wa kampeni ya elimu kwa mlipakodi
inayoendelea jijini humo. (PICHA ZOTE NA
VERONICA KAZIMOTO.)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...