Kaimu Mkuu wa Maabara wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) Kanda ya Ziwa Bugusu Nyamweru akizungumza na waandishi wa Habari waliotembelea Maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa.


*Ni Mashine ya Kisasa iliyopo katika Maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa 

Na Chalila Kibuda,Michuzi Tv

Mamlaka ya Dawa na  Vifaa Tiba  (TMDA) Kanda ya Ziwa  imesema mashine ya LC,MS/MS. ina umuhimu katika uchunguzi wa sumu na kemikali katika Mwili wa Binadamu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Katika Maabara ya TMDA Kanda ya Ziwa Kaimu Mkuu wa Maabara hiyo  Bugusu Nyamweru, amesema mashine  hiyo inafanya kazi na kuwa   msaada katika ukanda huo.

Amesema katika mashine hiyo wanafanya uchunguzi mbalimbali  pamoja na za utafiti za kawaida, chunguzi za kuangalia  au kutambua kiwango cha kemikali na dawa ndani ya mwili wa binadamu.

Aidha amesema mashine hiyo Ina uwezo wa kufanya uchunguzi kwa kung'amua vitu vidogo sana  katika Mwili wa Binadamu.

Hata hivyo amesema faida ya mashine hiyo wakati wa kufanya uchunguzi inauwezo wa kugundua vitu vidogo sana vilivyo katika mwili wa binadamu pamoja na kutambua kiasi  cha kemikali katika sampuli yeyote.

Amesema kwa kawaida uchunguzi unafanyika mara mbili hadi pale  kemikali imeweza kuchanganuliwa katika vipande ambapo mwisho  kupata  maumbile au kipande cha  kinachotokana na  bacteria wa aina fulani.

Nyamweru amesema kuwa mashine hiyo pia inaweza kutumika katika kupima uchafuzi katika dawa na mazingira ya dawa katika uhifadhi wake kwa kuangalia kiambata hai kwenye dawa.

Nyamweru amesema kuna kiambata kingine sio hai au kiambata hai kilichoharibika katika mwili.

“Tunafanya uchunguzi  wa dawa inavyofanya kazi katika mwilini na   hufanyika baada ya dawa kufika na mabaki yake kuangaliwa kwa  umbo gani na yametengenezwa kwa kemikali ipi au kujua kwamba dawa iliyotumika katika mwili  katika eneo fulani iko kwa kiasi gani katika mifumo ya  mkojo au mate au katika tishu ya mwili  na sehemu zingine kama kwenye Moyo,Ini iko kwa kiasi gani."amesema Nyamweru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...