Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
KITUO
 Cha kupozea umeme kilichopo Mlandizi ,mkoani Pwani kinatarajia kuongeza
 uwezo wa upatikanaji wa Umeme MVA 120 ,ifikapo mwezi march mwaka huu na
 baadae itaongezeka na kufikia MVA 240 kwa mwaka 2022.
Lengo
 kuu la kuongeza kasi katika upatikanaji wa nishati ya umeme imetokana 
na mahitaji makubwa ya umeme viwandani na majumbani kutoka 60 mwaka 2015
 na kufikia 117.8 mwaka huu.
Hayo
 yamebainika wakati mkuu wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo 
alipokwenda kutembelea kituo hicho ambacho kiliungua na kusababisha 
changamoto ya upungufu wa umeme ambapo kimefanyiwa maboresho na kuongeza
 transfoma itakayowashwa mwezi ujao na kuongeza upatikanaji wa umeme wa 
MVA 120.
Ndikilo alisema,
 ameridhishwa na kasi ya shirika la umeme Tanesco chini ya meneja 
mhandisi Mahawa Mkaka ,kutekeleza kwa vitendo mpango mkakati unaoendana 
na mahitaji ya umeme na hatimae kufikia adhma ya mkoa ya UKANDA wa 
viwanda .
"Kituo hiki 
kinapeleka pia umeme maeneo ya viwanda Zegereni kwenye viwanda 25 na 
majumbani, Bandari kavu ya Kwala na kina hudumia wateja 182,000 kati ya 
hao ni viwanda vya kati na vikubwa 322 ,hongereni sana 'alieleza Ndikilo
 .
Aidha,aliitaka Tanesco
 kushughulikia changamoto ya Mkuranga kuendelea kupata umeme kituo cha 
umeme Mbagala wakati wilaya hiyo imesheheni kwa viwanda hivyo iondokane 
na kutegemea umeme katika kituo hicho.
Hata
 hivyo Ndikilo alielekeza taasisi nyingine wezeshi ya DAWASA na ile 
inayohusika na barabara kuendana na kasi ya mkoa kuinua sekta ya 
uwekezaji kwa kufikisha huduma muhimu maeneo ya viwanda .
Awali
 akitoa taarifa ya utekelezaji na maboresho ,meneja wa Tanesco mkoani 
Pwani ,mhandisi Mahawa Mkaka alisema,mwaka 2018-2020 walikuwa 
wakihudumia viwanda 1,275.
"
 Tunaishukuru serikali ya awamu ya tano kwani tumeweza kuwa na miradi 
mingi ikiwemo mradi wa REA III awamu ya kwanza uliogharimu bilioni 37 na
 kufikia wateja zaidi ya 6,000,mradi wa Peri-Urban bilioni 65 na 
kuunganisha maeneo 178 na mradi wa ujazilizi ambao unatarajia kuanza 
bilioni 10 ambapo maeneo 116 yatafikiwa"alifafanua Mkaka.
Mkaka
 alieleza, miradi ya Tanesco kwa mwaka wa fedha 2021-2022 itagharimu 
bilioni 10.2 kwa ajili ya kuboresha sekta hiyo na kusogeza huduma ya 
umeme maeneo 121.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...