Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wengi wakijumuika na Wananchi wa Zanzibar katika Sala ya kuusalia mwili wa marehemu aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, ilioongozwa na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi, iliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar leo 18-2-2021.(Picha na Ikulu)
Makanali na Mameja wa JWTZ wakiwa wamebeka jeneza la Mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad uliopowasiliu Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar, kwa ajili ya kuagwa na Wananchi wa Zanzibar katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwa na Viongozi wakiaga baada ya kumalizika kwa Sala ya kumuimbea aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, iliofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi na Viongozi wa Dini na Serikali wakiitikia dua ikisomwa na Katibu wa Ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Abdalla Talib, baada ya kumalizika kwa Sala ya kuusalia mwili wa aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, iliofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar.
Baadhi ya wananchi wakiwa katika mazishi ya MaalimSeif (Picha na Ikulu)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...