Na Mwandishi wetu
Dar es Salaam. Jumla ya klabu tisa (9) za mchezo wa kuogelea zimethibitisha kushiriki katika mashindano ya Taliss yaliyopangwa kufanyika kwenye bwawa la kuogelea la klabu ya Gymkhana jijini Dar es Salaam.
Meneja wa klabu ya Taliss, Hadija Shebe amezitaja klabu hizo kuwa ni Dar es Salaam Swimming Club (DSC), Bluefins, Mis Piranhas, Champion Rise, UWC Moshi, Wahoo (Zanzibar) na wenyeji, Taliss. Pia zipo klabu za Bluefins, Mwanza Swimming Club na FK Blue Marlins.
Hadija alisema kuwa wanatarajia kuwa na mashindano yenye ushindani mkubwa kutokana na ukweli kuwa mashindano hayo ni ya kwanza tokea kuruhusiwa kwa michezo nchini Juni Mosi mwakani/
Alisema kuwa pamoja na serikali kuruhusu kuendelea kwa michezo, bado mchezo wa kuogelea ulishindwa kufanya shindano hapa moja kwa mujibu wa kalenda ya chama cha mchezo huo nchini kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wao.
“Waogeleaji walikuwa wanafanya mazoezi tu. Haya ndiyo mashindano ya kwanza kwa mujibu wa kalenda ya michezo ya TSA na hivyo tunatarajia ushindani mkubwa kutoka kwa waogeleaji ambao wamejifua kwa muda mrefu sana,” alisema Hadija.
Hadija alisema kuwa ili kuleta ushindani katika mashindano hayo, kila muogeleaji atatakiwa kuchagua kushindana kwenye aina sita ya mashindano na matukio mawili kwa ajili ya relay.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...