Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-Arusha 


Shirika la Umeme Tanesco limejipanga kuhakikisha umeme unafika maeneo yote  ambayo wananchi wanahitaji kwa lengo la kuendeleza uchumi wa wananchi ,mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla .

Hayo yamebainishwa na   kaimu meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha  Mnhandisi  Andrew Lucas Ako wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya nne ya mifuko ya programu uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika mkoani hapa Katika viwanja vya kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid, ambapo alisema kuwa  kwa upande  Arusha jiji wameweza kuunganisha umeme kwa wananchi kwa asilimia 80  , na  asilimia 20 iliobaki wanapambana kumalizia na wanaamini Katika awamu hii ya miaka mitano watamalizia asilimia zilizobaki.

Alibainisha kuwa  katika jitihada za kuisaidia serikali kuwezesha wananchi kiuchumi shirika la Umeme Tanesco  linahakikisha maeneo yote ambayo wananchi wanahitaji umeme ,yanawekwa  kwa bei nafuu na maeneo mengine wananchi wanawekewa umeme kwa gharama za Shirika  kutokana na uhitaji wa wananchi lengo kubwa ni kuhakikisha wanapata mahitaji yao ya msingi.

Alisema kuwa shirika la umeme Tanesco lipo Katika  maonesho hayo kwa ajili ya kutoa elimu kwa wananchi wote wanaofika katika maonesho hayo kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo ,pia wajue miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na tanesco mkoa wa Arusha .

"Sasa hivi tuna miradi  mikubwa na midogo ambayo tunatekeleza kama mkoa kwa bajeti ya mwaka 2020/2021 ,miradi midogo tunayotekeleza ina gharimu kihasi cha shilingi bilioni 10 kwa Arusha  na hadi sasa tumeshatekeleza kwa asilimia 80 na tunaamini adi ifike mwezi wa nne tutakuwa tumekamilisha "alibainisha Ako.

Akifungua maonyesho hayo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alivitaka  vyombo mbalimbali vya habari kushiriki kikamilifu katika maonesho hayo ili viweze kufikisha ujumbe sahihi kuhusu fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi kupitia mifuko na programu za uwezeshaji kwa wananchi wote nchini.

Alibainisha kuwa  tathmini za mara kwa mara zinazofanywa na Serikali kuhusu utendaji wa Mifuko na Program za Serikali za uwezeshaji zinaonesha kwamba mifuko hiyo na programu hizo zimechangia kwa kiwango kikubwa jitihada zake za kukuza uchumi na kupunguza umaskini..



wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanesco wakiwa katika banda lao lililopo Katika maonyesho  ya nne ya mifuko  programu uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika Katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha
Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco mkoa wa Arusha Mhandisi Andrew Lucas Ako akiongea na waandishi wa habari Katika maonyesho hayo

Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo wa kwanza kushoto akibadilishana mawazo na baadhi ya waandishi wa habari waliouhudhuria  maonesho ya nne ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...