Na Abdullatif Yunus Michuzi TV.

Katibu Mkuu Chama Cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) Ndg. Hery Mkunda, Ameendelea na Ziara yake Mkoani Kagera ikiwa ni Siku ya Pili, ambapo ametembelea Baadhi ya Matawi ya TUGHE ya Hospitali ya Rufaa Bukoba Mkoani Kagera, BUWASA, Bonde la Ziwa Victoria na Kisha kukutana na Wanachama, Viongozi wa Matawi pamoja naWaajiri kwenye Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera Februari 22, 2021.

Katika Kikao hicho, Katibu Mkuu Hery Mkunda amewakumbusha Wanachama hao wajibu wao Kama Wafanyakazi, ikiwa Ni pamoja na kujipanga na maisha baada ya kustaafu, likiwemo suala la Kikotoo, sambamba na kuwaomba Kuendeleza mahusiano mema Kati yao na Waajiri wao ili kuondoa misugano isiyokuwa ya lazima.

Mbali na Mambo mengine pia, Katibu Mkuu Hery Amesikiliza sehemu ya changamoto zilizowasilishwa katika Kikao hicho,  miongoni mwazo ikiwa ni malalamiko kuhusu suala la kupandishwa Vyeo kwa Baadhi ya Watumishi wenye sifa, kucheleweshwa kwa Pensheni, sambamba na Kupandisha mishahara ambayo kimekuwa ni kilio cha Miaka mingi Sasa, mengine yakuhusu suala la Bima ya Afya.

Miongoni mwa masuala yaliyowasilishwa katika Kikao hicho, Katibu Mkuu TUGHE Taifa Ndg. Hery Makunda ameahidi kuanza kuyashughulikia na pengine kupatiwa Ufumbuzi kabla ya Mei Mosi.


Katibu Mkuu TUGHE Taifa, Ndg. Hery Mkunda akizungumza na Wanachama pamoja na Viongozi katika Kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa Kagera Februari 2021
Katibu Mkuu TUGHE Taifa Ndg. Hery Mkunda akiongea na Wanachama Tawi la Bonde la Ziwa Victoria alipofika katika Ofisi zao.


Katibu Mkuu TUGHE Taifa Ndg. Hery akiteta na Katibu Tawala Mkoa Kagera Profesa Faustine Kamuzora alipofika Ofisini kwake Kujitambulisha

 Picha ya pamoja na Wanachama na  Katibu Mkuu TUGHE Taifa wakionesha ishara ya Mshikamano Daima.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...