Na. Beatrice Sanga-MAELEZO
BODI ya Utalii Tanzania (TTB) inatarajia kufanya maonesho ya
Kimataifa ya Utalii ( Swahili International Tourism Expo ) maarufu
kama “SITE” yatakayoanza Oktoba 8 hadi 10, 2021 Mlimani City Jijini
Dar es Salaam na kushirikisha Mawakala wa Utalii wa Kimataifa,
waandishi wa habari za utalii wa Kimataifa, na wafanyabiashara wa
utalii kutoka Tanzania na nchi za jirani.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii
Tanzania Bi Devota Mdachi, amesema Bodi kwa kushirikiana na Balozi
za Tanzania ng’ambo imejipanga kuwavutia mawakala wa utalii na
waandishi wa habari za utalii wa Kimataifa kutoka nchi zao za
uwakilishi pia kuvutia makampuni ya uoneshaji yapatayo 200 kutoka
Tanzania, Nchi za Afrika Mashariki, Kati, Kusini na Afrika Magharibi.
Tanzania Bi Devota Mdachi, amesema Bodi kwa kushirikiana na Balozi
za Tanzania ng’ambo imejipanga kuwavutia mawakala wa utalii na
waandishi wa habari za utalii wa Kimataifa kutoka nchi zao za
uwakilishi pia kuvutia makampuni ya uoneshaji yapatayo 200 kutoka
Tanzania, Nchi za Afrika Mashariki, Kati, Kusini na Afrika Magharibi.
“Kama kawaida yetu, onesho litakuwa na programu kadhaa zitakazo
ongeza mvuto kwa mawakala wa kimataifa wa utalii, lakini pia
tumejipanga kuendesha programu ya ziara ya mafunzo kwa baadhi ya
mawakala wa utalii na waandishi wa habari za utalii wa Kimataifa ,
onesho litakuwa na programu za semina mbalimbali ambazo pamoja
na masuala mengine zitalenga kutoa elimu kwa washiriki kuhusu
mikakati ya kuvutia watalii katika kipindi hiki cha Janga la Corona”,
amesema Mdachi.
Aliongeza kuwa, SITE ya mwaka huu inabeba umuhimu mkubwa na wa
kipekee kwa mawakala wote wa utalii wa Tanzania kwa kuzingatia
kuwa fursa za maonesho ya Kimataifa kama hayo bado hazijafunguka
katika nchi nyingine kwa sababu ya changamoto ya ugonjwa wa
Corona.
Amebainisha kuwa, TTB ina uhakika wa kuwapata mawakala wa
kimataifa, kutokana na makundi ya mawakala na watalii ambao
imekuwa ikiwaleta baada ya Tanzania kufungua anga ambapo mpaka
sasa Tanzania imeweza kupokea mawakala na watalii kutoka Nchi
mbalimbali kama Urusi, Ukraine, Poland, Czech, Japani, Uhispania,
Ufaransa, Uturuki na Uingereza .
Aidha, Mdachi ametoa wito kwa wadhamini, wadau, na wananchi kwa
ujumla kujitokeza kwa wingi kutembelea onesho hilo ikiwa ni sehemu
ya utalii wa ndani na kupata elimu kuhusu biashara za utalii lakini pia
makampuni ya biashara za hoteli na mawakala wa utalii kuweza
kutumia fursa zinazopatikana katika onesho hilo kwa ajili ya
kujitambulisha na kujitangaza zaidi katika sekta ya utalii.
“Makampuni yenye uwezo wa kudhamini onyesho hili napenda
kuwahakikishia kuwa udhamini wao kwa onesho la SITE ni fursa ya
kipekee kujitambulisha kwenye sekta ya utalii ambayo inamatumaini
makubwa kushamiri kwa kasi (To bounce back) mara dunia
itakapofunguka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...