Na Woinde Shizza , Michuzi Tv Arusha
KINYANG'ANYIRO cha uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi mbalimbali zilizoachwa wazi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM,) Mkoa wa Arusha baada ya makada kupata nafasi za Ubunge na udiwani umeanza kwa kasi ambapo makada 28 wamerudisha fomu za kuwania nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa (NEC) Mkoa wa Arusha .
Akizungumza na waandishi wa habari ofisni kwake Katibu wa CCM Mkoa wa Arusha, Musa Matoroka amesema kuwa zoezi la uchukuaji wa fomu lilianza mapema Februari 10 nakumalizika February 13 mwaka huu huku fomu hizo zikitolewa bure.
Akizungumzia nafasi ya MNEC Mkoa wa Arusha amesema kuwa makada 32 wamejitokeza kuchukua fomu na kati yao 28 ndio wamefanikiwa kurejesha.
Amesema nafasi nyingine zinazowaniwa ni Katibu itikadi na uenezi Wilaya ya Arusha na Karatu ambapo Kati ya wanachama 36 waliochukua fomu Wilaya ya Arusha na 34 wamerejesha, huku Wilaya ya Karatu waliochukua wakiwa 12 na wote wamerejesha.
Nafasi nyingine inayowaniwa ni Mwenyekiti wa wazazi Wilaya ya Karatu na Arumeru ambapo wanachama 5 waliojitokeza kuchukua fomu Wilaya ya Karatu na wote wamejeresha na katika Wilaya ya Arumeru 10 waLichukua fomu na wanachama tisa wamerejesha fomu hizo.
Pia katika wilaya ya Ngorongoro wanachama wa CCM 8 wamejitokeza kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa umoja wa wanawake UWT na wote wamerejesha fomu.
Matoroka ameongeza kuwa baada ya fomu hizo kurejeshwa upembuzi yakinifu utafuata ikiwemo baadhi ya nafasi za wagombea fomu zao kwenda makao makuu ya chama na nyingine kupitiwa na kamati mbalimbali Mkoani hapo na kupanga tarehe za uchaguzi.
Aidha metoa rai kwa makada hao kuacha kujihusisha na vitendo vya Rushwa au kufanya kampeni kabla ya kuruhusiwa na kwa yeyote atakayebainika chama kutafuta jina lake na kumchukulia hatua kali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...