Charles James, Michuzi TV

MBUNGE wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku 'Msukuma' amemuomba Rais Dk John Magufuli kukutana na wafanyabiashara nchini ili kujua changamoto wanazokutana nazo lengo likiwa kuweka mazingira bora ya kibiashara yatakayochangia ukuaji wa uchumi wa Nchi.

Msukuma ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia hotuba ya Waziri wa Fedha, Dk Philip Mpango ya Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti ya Serikali na Mpango wa Maendeleo ya Taifa pamoja na Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa miaka mitano 2021/22-2025/26.

Akichangia hotuba hiyo, Mbunge Msukuma amesema ni ukweli usio na shaka kwamba wananchi wamekua wakilalamikia ugumu wa maisha huku wafanyabiashara wakifunga maduka na biashara zao yote hayo akisema yanachangiwa na sheria za kodi ambazo sio rafiki.

" Nimuombe Rais Magufuli kama alivyokaa na sisi wadau wa Madini basi tunamuomba akae na wafanyabiashara wamueleze changamoto zao naamini baada ya hapo watakua wamepiga hatua kubwa sana ya kujua namna gani ya kuinua uchumi wetu.

Hawa vijana wanaomaliza vyuo vikuu wanalalamika hakuna fedha na ajira mitaani , kama tumeweza kuwakopesha elimu kwa kuwapa mikopo ya Chuo kwanini tusiweke mazingira mazuri ya Mabenki yetu kuwakopesha vijana hawa na dhamana yao iwe vyeti vyao? Hiyo itachangia sana kumaliza changamoto ya ajira nchini," Amesema Msukuma.

Ameishauri Serikali kuacha kutumia fedha nyingi katika miradi ambayo haina manufaa yoyote kwa wananchi na badala yake imekua ikiitia serikali hasara akitolea mfano ujenzi wa Masoko kama Soko la Ndugai jijini Dodoma, Soko la Morogoro na Machinga Complex jijini Dar es Salaam.

" Hatuwezi kupambana kujenga uchumi wa Nchi yetu huku tukiangaika na miradi ambayo haiiletei faida Nchi yetu, masoko kama Soko la Ndugai, Machinga Complex ni hasara kubwa licha ya kutumia mabilioni mengi kuyajenga, ukienda pale hakuna watu niombe serikali iache kufanya miradi ya namna hii," Amesema Mbunge Msukuma.

MBUNGE wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Kasheku 'Msukuma'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...