Charles James, Michuzi TV
UTALII na Kilimo! Ndio Sekta ambazo Mbunge wa Jimbo la Gairo Mkoani Morogoro, Ahmed Shabiby anaamini zinaweza kuchangia ukuaji wa uchumi wa Nchi yetu huku akitaka nguvu kubwa iwekwe kwenye matangazo ya utalii.
Shabiby ameyasema hayo leo bungeni jijini Dodoma alipokua akichangia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ya Mapendekezo ya Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa kwa miaka mitano ambapo ametoa wito kwa Serikali kuweka waambata biashara kwenye kila Balozi zetu kwa ajili ya kutangaza vivutio vyetu vya utalii.
Amesema Tanzania ndio Nchi ya pili kwa utalii duniani nyuma ya Brazil lakini imeshindwa kutangaza vivutio vyake kiasi cha kuzidiwa hata na Nchi ambazo hazina vivutio vingi na vizuri.
" Brazil wanaongoza lakini wanategemea utalii wa Bahari tu sisi tuna kila kitu ambacho wenzetu hawana, leo hii Masai Mara inatangazwa zaidi ya Serengeti, wageni wakija wanafikia Kenya wanapita Masai Mara ndio waje Serengeti, hata Mlima Kilimanjaro unatangazwa zaidi Kenya kuliko sisi tunavyoutangaza.
Kuhusu sekta ya Kilimo, Shabiby amesema kama serikali itaendelea kudharau sekta hiyo basi ni ngumu sana kuendelea kukua kiuchumi kwa sababu asilimia 70 ya uchumi wetu unategemea kilimo.
Amesema kwa miaka mingi serikali imekua ikibadilisha kauli mbiu za kilimo lakini hakuna jitihada zozote za kuboresha sekta hiyo na kuinua wakulima huku akisema Wizara ya Fedha imekua haitoi fedha za kutosha kwa Wizara ya Kilimo.
" Ni jambo la aibu kuona Tanzania tunaagiza bidhaa zinazotokana na mazao Nje ya Nchi, mfano Saudia Arabia ambayo inapata mvua mara moja tu kwa mwaka inalima Tani Laki Saba za Ngano sisi ambao kila siku tunapata mvua hadi tunalalamika ndio kwanza tunaagiza kwao.
Tunamaliza fedha nyingi kuagiza mazao ambayo sisi tunaweza kuyalima, Alizeti hapa kwetu inakubali ila ndio kwanza tunaagiza Malaysia, ni lazima tufike sehemu tuseme ukweli Wizara ya Fedha haitoi bajeti ya kutosha kwa Wizara ya Kilimo tutaishia kubadilisha 'slogan' tu kila siku mara Kilimo ni Uti wa Mgongo, Kilimo cha Kibiashara lakini kama hatuweki mikakati ya kutosha hatutopiga hatua," Amesema Shabiby.
Home
UTALII WETU
SHABIBY AITOLEA UVIVU WIZARA YA UTALII, AITAKA KUWEKA MIKAKATI YA KUTANGAZA VIVUTIO VILIVYOPO NCHINI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...