Mifumo ya Taka Sifuri yaweza tengeneza ajira zaidi ya 18,000 kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam.
Taka Sifuri ukionekana ni mkakati muhimu katika kutengeneza uchumi imara na endelevu baada ya COVID-19
Tafiti mpya kutoka GAIA imeonyesha kuwa miji inayowekeza kwenye miradi ya taka sifuri na sera inatengeneza ajira nyingi kijani, ikiwa na faida kubwa pia ya kupunguza uharibifu na uchafuzi wa mazingira na kuboresha afya ya jamii.
Ripoti hii imekuja wakati serikali za manispaa mbalimbali duniani zikiwa zinachukua maamuzi juu ya miradi gani ya kiuwekezaji ifanyike ili kuongeza ustahimilivu wa hali ya hewa na kuujenga upya uchumi ambayo umeathiriwa na janga
la COVID-19.
Tafiti imetazamia kuwa kama jiji la Dar es Salaam lingerejesha asilimia 80 ya taka
rejeshi ndani ya taka zizalishwazo, jiji linauwezo wa kutengeneza ajira mpya aidi ya 18,000.
Katika uchambuzi wa meta ya kimataifa wa uwezekano wa kutengeneza ajira wa sekta tofauti za usimamizi wa taka, utafiti unaweka wazi kuwa kilicho kizuri kwa mazingira pia ni kizuri kwa uchumi.Mikakati ya taka sifuri imepata maksi za juu zaidi kwenye faida za kimazingira na utengeneza ajira nyingi kupitia eneo lolote la usimamizi wa taka:
Utumiaji tena yaani reuse utengeneza zaidi ya mara 200 ya ajira kuliko madampo na
uchomaji. Urejeleshaji utengeneza karibu mara 70 ya ajira kuliko madampo na uchomaji. Utengenezaji upya utengeneza kiasi cha mara 30 zaidi ya ajira kuliko madampo na
uchomaji.
Taka sifuri ni mfumo thabiti wa usimamizi wa taka ambao unatoa kipaumbele cha kupunguza taka na urejeshaji vifaakazi, kwa lengo la kujenga uchumi imara, kuondoa utupaji wa taka kufikia sifuri.
Kwa upande mwingine, mifumo ya utupaji inategemea na uchomaji ("taka kwa nishati") na madampo ili kukabiliana na vyanzo vingi vya taka, na kusababisha gharama kubwa za kiuchumi na matokeo ya kimazingira.
Mifumo ya taka sifuri sio tu inatengeneza ajira nyingi, inatengeneza ajira zilizo bora. Tafiti
zinaonyesha kuwa ajira katika mifumo ya taka sifuri huenda zaidi ya kazi za mikono, utoa mishahara ya juu, utoa nafasi zaidi za kudumu, na kuboresha ubora wa maisha.
Kwa mfano, mfumo wa kibubunifu wa taka sifuri ambao unatekelezwa na taasisi ya ndani
isiyotengeneza faida, Nipe Fagio katika jamii zenye kipato cha chini jijini Dar es Salaam unaendana na usimamizi wa mazingira na ujumuishaji wa jamii kwa kufanya kazi na watu walio katika mazingira magumu na kuishirikisha jamii katika ufumbuzi mzuri na wa gharama nafuu. Unapunguza kazi kubwa ya usimamizi wa taka kwa mfumo kuwekwa kipekee kwenye eneo halisi la jamii.
Ana Le Rocha, Mkurugenzi Mtendaji wa Nipe Fagio alisema, “Mfumo wa Taka Sifuri jijini Dar es Salaam una uwezo wa kutengeneza ajira 40 katika kila jamii yenye kaya 5,000 kwa makadirio, kwa kuzalisha kipato ndani ya jamii na kuzidi kuleta matokeo chanya katika kuijengea jamii uwezo na elimu.”
Aidha, mwandishi wa ripoti hiyo, Dk. Neil Tangri, ambaye ni Mkurugenzi wa Sera na Sayansi kutoka GAIA alisema, “dunia ikiwa bado katika vita dhidi ya janga, utengenezaji wa ajira ni kipaumbele kikubwa. Mfumo wa taka sifuri unatoa mkakati mzuri wa kutengeneza ajira borana kupunguza uchafuzi na uharibifu wa mazingira. Ni ushindi mara tatu kwa uchumi, mazingira, na jiji kwa ujumla.”
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...