Naibu Waziri wa Maji Mhandisi  Maryprisca Mahundi (Mb)amezindua mradi wa maji Kijiji cha Mwabaratulu Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba Mkoani Mwanza ulioghalimu shilingi milioni 177.

Pichani Naibu Waziri Maryprisca Mahundi akimtua ndoo mama kichwani katika kijiji cha Mwabaratulu  Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba ikiwa ni ishara ya kumalizwa kero ya maji katika Kijiji hicho.

Aidha wananchi wamepewa mwezi mmoja kutumia maji bure bila malipo.

Hata hivyo Naibu Waziri amewataka kutunza miundo mbinu ya maji ili serikali ifikie malengo yake sambamba na kumtua mama ndoo kichwani kwani wanawake ndiyo wahanga wakubwa ikiwa ni pamoja na migogoro katika ndoa.

"Mheshimiwa Rais Magufuli ametoa pesa nyingi katika miradi ya maji nchini hivyo wataalamu na wananchi tunapaswa kushirikiana ili kuifikia matamanio ya Rais kuona kila Mtanzania anakunywa maji safi na salama" alisema Naibu Waziri wa Maji.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...