*Ni katika ukarabati wa ofisi ya kutolea huduma za za vifurushi.
*Thamani ya mradi ni bilioni moja ,thamani ya mradi ya fedha sh.milioni 400

Na Chalila Kibuda ,Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari, Mhandisi Kundo Andrea aibua ubadhirifu wa fedha za Umma kwenye ukarabati wa Jengo la Shirika la posta unaodaiwa kugharibu shilingi bilioni moja.

Naibu Waziri huyo aliyasema hayo wakati alipofanya ziara makao Makuu ya Shirika la Posta katika eneo la ukarabati wa ofisi za kutolea huduma za vifurushi Posta Mpya jijini Dar es Salaam.

Amesema Rais anapambana kupata fedha kwa ajili ya wananchi wanyonge lakini baadhi ya watumishi wanafuja fedha hizo kwa ukarabati usiondana thamani ya fedha kutokana na shirika hilo kushindwa kusimamia na kusababisha mkandarasi kulipua.

Mhandisi Kundo amesema kuwa ukarabati wa jengo la posta umegubikwa usanii mwingi katika ukarabati wa jengo ambapo ameongeza kuwa usanii uliokuwa ukifanywa sasa basi hakuna nyongeza ya kufanya usanii huo.

Amesema kuwa kwa mradi wa ukarabati wa jengo hilo thamani halisi ni sh.milioni 400 hivyo sh.milioni 600 lazima zirudi ili ziweze kufanya kazi hata kujenga daraja au hospitali kwani wananchi bado wanashida na hivyo vitu.

Naibu Waziri huyo amesema katika kipindi hiki hakuna mtu ataachwa salama ikiwemo Posta kwa fedha iliyofanya ukarabati isioendana na thamani kabisa huku menejimenti ya shirika ikiwa haina hata habari.

Aidha amesema Meneja mkuu wa Shirika la Posta kuwa mwangalifu kusiwepo na watu wa kumzunguka kwa vitu vidogo kwani anatakiwa kuangalia baadaye kushika nyadhifa zingine kutokana na umri wake na hakuna anayetambua kuwa baadaye anaweza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Mhandisi Kundo amesema kuwa taarifa za shirika hilo anazo hivyo hakuna mtu wa kuweza kumdanganya katika kuficha ukarabati wa ujenzi huo na namna mkandarasi aliyepatikana katika kuchukua zabuni hiyo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Habari na Teknolojia Mhandisi Kundo Andrea akimunesha Meneja Mkuu wa Shirika la Posta namna alivyokarabati jengo chini ya kiwango.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Habari na Teknolojia Mhandisi Kundo Andrea akionesha Taa iiyowekwa ni ya kawaida gharama yake iko juu na haiendani na taratibu za manunuzi.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, habari na Teknolojia Mhandisi Kundo Andrea akizungumza na waandishi wa habari kuhusiama na ukarabati wa jengo la posta usioendana na thamani ya fedha lililopo Posta Mpya jijini Dar es Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...