MKOA wa Ruvuma umepokea
shilingi 9,205,781,600.28 ili kutekeleza sera ya utoaji elimu bila malipo
katika kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Desemba 2019 hadi Novemba 2020.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
Christina Mndeme amesema fedha hizo zimesaidia kuongeza kiwango cha
uandikishaji na mahudhurio ya wanafunzi katika shule za msingi na sekondari
ikiwa ni pamoja na kuongezeka upatikanaji wa vitabu vya kiada na ziada.
“Utekelezaji wa sera
hii umeweza kuleta unafuu kwa wazazi na walezi katika kugharamia gharama za
elimu kwa watoto wao’’,alisisitiza Mndeme.
Mndeme amesema Mkoa
umeendelea kuimarisha utoaji wa elimu katika ngazi zote na kwamba Mkoa wa
Ruvuma umepata mafanikio makubwa baada ya serikali kujenga vyuo viwili vipya vya ufundi stadi VETA na kuufanya Mkoa
kuwa na vyuo vitatu vya VETA.
Hata hivyo amesema Mkoa
hivi sasa unaweka msukumo mkubwa katika utoaji wa taaluma bora kwa
kuwashirikisha wadau wote wa elimu ili kuhakikisha kila mdau anashiriki kufanikisha
tendo la ufundishaji,ujifunzaji na mahudhurio ya wanafunzi shuleni.
“Kwa niaba ya wananchi,naishukuru serikali ya
Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wetu Mhe.Dkt.John Magufuli kwa kuendelea
kufanya elimu kuwa kipaumbele ambapo serikali imeamua kila Mkoa,ukiwemo Mkoa
wetu kujenga shule moja ya sekondari ya wasichana ya kitaifa’’,alisema Mndeme.
Mkoa wa Ruvuma una jumla ya shule za msingi
808 kati ya hizo,shule za serikali ni 778 na zisizo za serikali 30,pia Mkoa una
shule za sekondari 206 kati ya hizo za serikali ni 150 na sekondari binafsi 56.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...