Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Abbas Tarimba (wa kwanza kutoka kushoto) akishika mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 120/- za Kitanzania ikiwa ni udhamini wa Kampuni hiyo kwa Namungo FC, Wa Kulia ni Mwenyekiti wa timu hiyo, Hassan Zidadu na wa katikati ni Mchezaji wa Namungo, Stephen Sey. Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Abbas Tarimba (wa kwanza kutoka kushoto) akisaini mkataba wa udhamini wa Shilingi za Kitanzania Milioni 120/-  na Namungo FC ya Ruangwa, Lindi (wa kati kati) ni Mwenyekiti wa Namungo FC, Hassan Zidadu, hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.

Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
KLABU ya Soka ya Namungo ya Ruangwa mkoni Lindi imelamba kitita cha Shilingi Milioni 120 za Kitanzania kutoka Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa Tanzania ikiwa ni pesa ya kujiweka sawa na kuendeleza mapambano katika msimu huu wa Mashindano.

Akizungumza wakati wa kukabidhi Hundi ya kiasi hicho kwa Mwannyeti wa Namungo, Mkurugenzi wa Utawala na Udhibiti wa SportPesa, Abbas Tarimba amesema wataendelea na udhamini huo kadri watakavyoweza kwa Namungo FC sambamba na timu za Simba SC, Yanga SC ili kuinua mpira wa Tanzania na baadae kuwa na timu bora ya Taifa.

Tarimba amesema SportPesa ina furahi mahusiano hayo ya  udhamini kwa timu zote ambazo itoa udhamini, amesema wana furaha kuona Yanga SC kuongoza Ligi Kuu Soka Tanzania Bara na Simba SC inayofanya vizuri Kimataifa.

"Namungo ina viporo vyake ikifanya vizuri itakuwa nafasi nzuri katika Ligi yetu na Kimataifa pia ina mchezo wake wa Mashindano ya Kombe la Shrikisho la Afrika dhidi ya CD Agosto ya Angola." Amesema Tarimba

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Namungo FC, Hassan Zidadu ameshukuru kwa udhamini huo msimu huu kwa timu hiyo na kuleta chachu ya mafanikio kwa timu hiyo.

"Tutajitahi kufanya vizuri kwenye Michuano ya Kimataifa ili kuishawishi SportPesa kuwa wadhamini wakuu wa Klabu yetu, kwa kweli mafanikio haya kwa kiasi kikubwa yamechagizwa na hawa SportPesa." Amesema Zidadu

Zidadu amesema watajitadi kufanya vizuri zaidi kupata mafanikio makubwa sambamba pia na kupata ushauri katika msuala mbalimbali kutoka SportPesa na Wadamini wengine.

"Namungo FC bado tunaendelea kuiomba SportPesa kuwa Wadhamini wetu wakuu, naamini maombi yetu yatafanikiwa kutokana na mazunguzo yetu sisi Namungo na wao." Ameeleza Zidadu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...