Na Munir Shemweta, WANMM MISENYI
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
amelitaka Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kukamilisha haraka mradi wake
wa jengo lake la Kitega uchumi lililopo Mutukula wilaya ya Misenyi mkoa
wa Kagera.
Akiwa katika
ziara yake ya siku moja katika mkoa wa Kagera kukagua utendaji kazi wa
sekta ya ardhi na miradi inayojengwa na NHC, Dkt Mabula alisema
kukamilika mapema kwa jengo la kitega uchumi katika eneo la Mutukula
siyo tu litaliwezesha shirika kupata fedha lakini litakuwa kichocheo cha
wafanyabiashara wa Tanzania na Uganda.
"Mradi
huu uko kistrategic ukikamilika tutapata wawekezaji na kasi ya
wafanyabiashara kukimbilia upande wa pili itapungua hivyo nataka jengo
hili liishe kufikia machi mwaka huu" alisema Dkt Mabula.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ujenzi
wa mradi wa kitega uchumi cha Mutukula umechukua muda mrefu na
kusisitiza kuwa, kutokana na maendeleo mazuri ya ujenzi ni matumaini
yake ujenzi wa mradi huo sasa utakamilika kwa wakati .
Alisema,
mradi huo wa kitega uchumi cha Mutukula ni kama njia ya Shirika la
Nyumba la Taifa kujenga majengo maengine ya biashara katika maeneo
mengine na kuongeza kuwa miradi kama hiyo italisaidia sana Shirika
kimapato.
Kwa upande wake
Meneja Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw.
Muungano Saguya alisema, shirika lake lina mkakati wa kujenga majengo ya
kibiashara katika maeneo ya mipakani ili kuimarisha biashara katika
maeneo hayo.
Aliongeza
kuwa, pamoja na NHC kuendelea na ujenzi wa mradi wake katika eneo la
Mutukula Shirika hilo liko katika mkakati wa kujenga vitega uchumi
vingime katika meneo yote ya mipaka ya Tanzania na nchi zingine na
kipaumbele kikiwa ni mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Sirari na
Tanzania na Zambia, Tunduma.
Msimamizi
wa mradi wa Kitega uchumi cha Mutukula mkoani Kagera Mhandisi George
Shanali alimueleza Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
kuwa mradi wa jengo hilo unaendelea vizuri na unatarajiwa kukamilika
Machi 15, 2021.
Alisema, mradi huo unaogharimu takriban bilioni 2.9 utajumuisha huduma za kibenki na maduka 36 ya biashara.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Jengo la Kitega uchumi cha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliopo Mutukula wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera tarehe 17 Februari 2021. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali Denice Mwila na kushoto ni Meneja Uhusiano na Huduma za Jamii Bw. Muungano Safuya.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa Jengo la Kitega uchumi cha Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) uliopo Mutukula wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera tarehe 17 Februari 2021. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Misenyi Kanali Denice Mwila na kushoto ni Meneja Uhusiano na Huduma za Jamii Bw. Muungano Safuya.
Sehemu ya jengo la Kitenga uchumi cha Shirika la Nyumba la Taifa lililopo Mutukula wilaya ya Misenyi mkoa wa Kagera.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...