MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam  Aboubakar Kunenge ameonesha kuchukizwa na kitendo cha kusuasua kwa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kinondoni Studio kuelekea Mwananyamala yenye urefu wa Km 4.2 jambo linalopelekea usumbufu kwa Wananchi hususani wagonjwa wanaokwenda kupata huduma Hospital ya Rufaa ya Mwananyamala.

Kutokana na hilo RC Kunenge amemtaka Mkandarasi anaetekeleza Mradi huo kutoka Kampuni ya CRSG kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili ifikapo July 30 Barabara iwe imekamilika kwa asilimia  100 na amesema ndani ya Mwezi mmoja kuanzia leo atarudi kukagua maendeleo ya Ujenzi.

Aidha RC Kunenge amewaonya TARURA kutokumuongezea muda Mkandarasi huyo ambapo pia amewaelekeza kuwa wakali na kusimamia kikamilifu mradi huo.

Miongoni mwa Mambo yaliyomkwaza zaidi RC Kunenge ni kuona hadi kufikia Sasa muda wa Mradi umefikia asilimia 62 lakini kazi iliyofanyika ni asilimia 16 huku wahusika wakitoa sababu dhaifu.

Kwa upande wake Makamu Mhandisi Mshauri wa Mradi huo kutoka Kampuni ya HP Gauf Wile John amemuahidi Mkuu wa Mkoa kuwa maagizo aliyotoa watayatekeleza kwa Wakati.

Ujenzi wa Barabara ya Kinondoni studio kuelekea Mwananyamala yenye urefu wa Km 4.2 inatekelezwa na Mkandarasi kutoka Kampuni ya CRSG.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...