Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb) akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa wa Msumbiji ulipokuwa ukipigwa wakati wa ufunguzi wa kikao cha Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC-TROIKA) kilichofanyika kwa njia ya mtandao . Kikao hicho kilijumuisha nchi za Msumbiji Mwenyekiti, Tanzania Mwenyekiti aliyepita na Malawi Mwenyekiti ajaye, |
=== ===== ======
Kikao
cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Utatu wa Jumuiya ya Maendeleo ya nchi
za Kusini mwa Afrika (SADC- TROIKA ) kilichofanyika kwa njia ya Mtandao
kimeridhia mapendekezo ya Mawaziri wa Afya wa SADC kutaka kikao cha
Baraza la Mawaziri wa SADC kifanyike kwa njia ya Mtandao ili kukabiliana
na janga la ugonjwa wa COVID 19 katika ukanda wake.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William
Ole Nasha (Mb) aliyeshiriki kikao hicho cha SADC Troika akimuwakilisha
Waziri wa Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki amesema kikao
hicho kilikutana kwa ajili ya kupitia na kujadili mapendekezo ya
Mawaziri wa afya wa SADC kilichofanyika Februari 29, 2021.
Amesema
Mawaziri wa Afya walipendekeza kuwa kikao cha Baraza la Mawaziri
kifanyike kwa njia ya mtandao na kikao cha Wakuu wa Nchi kilichokuwa
kifanyike mwezi Machi kisogezwe mbele ambapo sasa kitafanyika kati ya
mwezi Mei au Juni kutegemeana na hali ya maambukizi ya ugonjwa wa COVID
19 itakavyokuwa na kuongeza kuwa vikao vingine vyote vitafanyika kwa
njia ya mtandao hadi hapo hali ya maambukizi itakapokuwa imetengemaa.
Vikao hivyo viwili vilikuwa vifanyike mwezi Machi ana kwa ana nchini Msumbiji
Utatu
wa SADC-TROIKA kwa sasa unaundwa na nchi za Msumbiji, Tanzania na
Malawi umefanya lichofanyika kwa njia ya mtandao kulikutana kujadili
taarifa ya kikao cha Mawaziri wa Afya wa SADC kilichokaa tarehe 29
Februari kuangalia hali ya ugonjwa wa COVID 19 katika ukanda wa SADC
ambacho kiliamua kuwa kikao cha Baraza la Mawaziri kifanyike kwa njia ya
Mtandao
Kikao
hicho kilitanguliwa na kikao cha maafsa waandamizi ambapo Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge alishiriki kikao hicho ambacho pia
kilifanyika kwa njia ya Mtandao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...