
Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
NI mchezo mkali wa kukata na Shoka baina ya Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Simba SC na miamba ya Soka Afrika, Al Ahly SC kutoka Misri, mchezo wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi utakaopigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kuelekea mchezo huo, Simba SC dhidi ya Al Ahly timu zote zimejinasibu kufanya vizuri ili kujiweka sawa katika Kundi A la Michuano hiyo.
Akizungumza kuekea mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Matola amekiri kuwa sio mchezo rahisi kutoka na ubora wa Al Ahly kwa sasa, amesema Simba SC imejipanga kufanya vizuri kufanya vizuri ili kujiweka sawa katika Kundi lake.
“Hii ni Ligi ya Mabingwa Afrika hakuna timu nyepesi, timu zote ni ngumu na michezo yote ni migumu, lakini lazima tupate matokeo mazuri”, amesema Matola
Matola amesema Wachezaji wote wako vizuri kuelekea mchezo huo, ameeleza hakuna majeruhi, “tunasubiri kesho kujua nani na nani wanaanza ili kuiwakilisha Simba SC vizuri katika mchezo huo”.
Kwa upande wake, Nahodha wa Kikosi cha Simba SC, John Bocco amesema wachezaji wote wamejipanga vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri, amesema Simba SC wataingia katika mchezo huo kuwaheshimu wapinzani wao, Al Ahly kutokana na ubora wao.
Kocha Mkuu wa Al Ahly SC, Pitso Mosimane amesema wataingia katika mchezo huo kupata matokeo mazuri ili kujiweka vizuri katika msimamo wa Kundi lao na baadae kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Michuano hiyo kama walivyofanya msimu uliopita.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...