Na Grace Semfuko, MAELEZO

Benki Kuu ya Tanzania-BOT imesema Waandishi wa Habari wanayo kazi kubwa ya kuelimisha jamii kuhusiana na hali halisi na mapitio ya Uchumi wa Tanzania na hivyo ipo haja ya kuwa weledi katika kufikisha taarifa kwa Umma.

Imesema Kutokana na kuwepo kwa ongezeko kubwa la ukuaji wa Uchumi nchini ni muhimu Watanzania wakaelimishwa kupitia vyombo vya Habari ambavyo vimekuwa na mchango Mkubwa katika uchumi wa Taifa na ustawi wa Kijamii.

Akifungua Semina ya Waandishi wa Habari za Biashara, Uchumi na Fedha, Kaimu Mkurugenzi wa BoT Tawi la Mtwara ambaye pia ni Meneja wa Utawala na Fedha Bw. David Mponeja amesema Kutokana na kuona umuhimu huo benki hiyo imeona ipo haja ya kuandaa semina hiyo.

“Tumieni weledi wenu kuwafahamisha wananchi hatua mbalimbali ambazo Serikali ya awamu ya tano katika kipindi hiki cha pili inazichukua katika kuwatumikia, waelezeni Wananchi hatua ambazo miradi ya kimkakati kama reli ya kisasa ya SGR, Ujenzi wa Mradi mkubwa wa kufua Umeme wa Rufiji na miradi mingine mingi ambayo kimsingi ndio ukuaji wa Uchumi halisi kwa sababu ikikamilika mambo yatakuwa mazuri" alisema.

Aliwataka Wananchi wanaohitaji kutoa huduma ndogondogo za Fedha kujisali na kujiandikisha kwa mamlaka mbalimbali kwa mujibu ya Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 ili waweze kutoa huduma hizo.

Aidha alisisitiza kuwa Benki hiyo itaendelea kushirikiana na vyombo vya habari ili kuhakikisha taarifa muhimu za BoT zinawafikia Wananchi.

Kaimu Mkurugenzi wa BoT Tawi la Mtwara ambaye pia ni Meneja wa Utawala na Fedha Bw. David Mponeja akisoma hotuba kwa niaba ya Mgeni rasmi Naibu Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT),Bwa. Julian Banzi wakati akifungua semina ya siku tano ya Waandishi wa Habari za Uchumi,Biashara na Fedha inayofanyika katika tawi la Benki Kuu mkoani Mtwara.
Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano (BoT),Vicky Msina akimkaribisha Mgeni rasmi
Kaimu Mkurugenzi wa BoT Tawi la Mtwara ambaye pia ni Meneja wa Utawala na Fedha Bw. David Mponeja (wa tatu kulia) kufungua semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha katika tawi la Benki Kuu Mtwara kwa niaba ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Bwa. Julian Banza leo Mkoani humo.
Meneja Msaidizi Idara ya uchumi Benki Kuu,Tawi la Mtwara,Aristedes Mrema akiwasilisha mada kuhusu Mwenendo wa Uchumi wa Tanzania pamoja na Tanzania kuwa ndani ya uchumi wa Kati katika Semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha iliofanyika leo katika tawi la Benki Kuu Mtwara.Mkuu wa Maendeleo ya Uchumi BoT Bw.Mussa Mziya akiwasilisha Mada katika Semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha uliofanyika leo katika tawi la Benki Kuu Mtwara.



Waandishi wa habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa katika semina hiyo inayohusu habari za uchumi, biashara na fedha katika ukumbi wa mkutano tawi la Benki Kuu Mtwara.
Mkuu wa Maendeleo ya Uchumi BOT Bw.Mussa Mziya akiwasilisha Mada katika Semina ya waandishi wa habari za uchumi, biashara na fedha uliofanyika leo katika tawi la Benki Kuu Mtwara.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...