Charles James, Michuzi TV
SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewaapisha wabunge watano kutoka Baraza la Wawakilishi kuwa Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ambavyo Katiba inaelekeza.
Wabunge hao ni Amein Abdallah Ameir, Bakari Hamad Bakari, Bahati Khamis Kombo, Mwantatu Mbarak Khamis na Suleiman Haroub Suleiman.
" Leo Wabunge watano wamekula kiapo cha uaminifu baada ya kupokea waraka wa Spika wa Bunge la Wawakilishi Zanzibar, Zuberi Ali Maulid kama ambavyo Katiba yetu inataka wabunge watano kutoka Baraza la Wawakilishi wawe sehemu ya bunge letu, sasa nafasi zilizobakia ni zile za Rais tu," Amesema Spika Ndugai.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...