Charles James, Michuzi TV

SERIKALI imewatoa wito kwa watanzania kukimbilia fursa ya kufundisha lugha ya Kiswahili Nje ya Nchi ikiwa ni baada ya lugha hiyo adhimu kukua kwa kasi hadi kwenye mataifa makubwa.

Wito huo umetolewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima aliehoji jitihada ambazo serikali imezichukua katika kukuza kiswahili duniani.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema kwa kufahamu mwamko wa lugha hiyo kwenye mataifa mengine tayari serikali imeziagiza Balozi zake zote kuwa na kituo maalum cha kufundishia lugha ya kiswahili lengo likiwa ni kupanua lugha hiyo.

" Ni kweli kiswahili kinazidi kukua na kushika kasi hadi kwenye mataifa makubwa kiasi kwamba hata Televisheni na Radio kubwa zimeanzisha vipindi vyao mahususi ambavyo vinafanywa kwa lugha ya kiswahili.

Kwa kutambua fursa ya kiswahili katika kukuza uchumi tumeagiza Balozi zetu kuwa na vituo hivyo ambapo sasa watanzania watapata fursa ya kwenda kuwa walimu jambo ambalo litapunguza changamoto ya ajira na kuiletea nchi yetu pia mapato," Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.



 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...