JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwakamata raia wa Burundi 05 wakiwa na watoto wao 05 kwa kosa la kuingia nchini bila kufuata taratibu za nchi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya SACP Ulrich O. Matei imeeleza kwamba tarehe 10.02.2021 majira ya saa 12:30 mchana huko kijiji na kata ya Changalawe, Tarafa Kiwanja, wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya . Askari Polisi wakiwa doria walisimamisha Basi la abiria yenye namba T.353 ANS inayomilikiwa na Kampuni AN ikitokea Mkoa Tabora kwenda Mbeya.
Askari walianza kufanya
ukaguzi kwenye basi hilo na ndipo walimkamata NDAYIPEUKAMIYE SADOCK [37] Raia
na Mkazi wa nchini Burundi akiwa na wenzake 04 pamoja na watoto wao 05
kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. Taratibu za kuwafikisha mahakamani
zinaendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...