Na Chalila Kibuda, Michuzi Tv
CHAMA cha Waandishi wa Habari Wanawake (TAMWA) kimekutanisha waandishi Habari kujadili rushwa ya ngono katika vyombo vya habari ambapo waandishi wamesema ipo kwa kiasi kikubwa lakini hakuna mfumo wa ndani wa kutoa taarifa.
Waandishi hao wamesema kuwa TAMWA imekuja wakati muafaka katika kulinda taaluma na kuweza kulinda jamii kwa ukubwa.
Akizungumza na waandishi Habari mara baada ya kuchechemua mada ya rushwa ya ngono katika Vyombo vya Habari Mkurugenzi wa Tamwa Rose Reuben amesema kuwa, waandishi wakionesha umahiri wa kuvunja ukimya wa rushwa ya ngono kutabadili Tanzania isiyo na rushwa na ngono.
Reuben amesema wameanza na waandishi kwa kutambua kundi muhimu ambalo hata linaweza liko tatizo la rushwa ya ngono.
Amesema rushwa ya ngono haidhibitiwi kwa mtu kuacha kazi kwani mtu anayefanya ataendelea kuwafanyia wengine.
"Tumeamua kuanza na kundi la waandishi kwa kutambua ndio wadau wa uelimishaji jamii na kuwaacha kuzungumza nao wakati wanaofanyiwa rushwa ya ngono." Amesema Reuben
Pia Mwenyekiti Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) Irene Mark amesema TAMWA imefungua ukurasa ambao baadaye kutaleta matokeo.
Mark amesema kuwa waandishi wa habari wametakiwa kuvunja ukimya kwa kutoa taarifa ili kuweza kukomesha rushwa ya ngono ndani ya vyombo vya habari.
Aidha Mkuu wa Dawati la Jinsi wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Leah Mbunda amesema kuwa Dawati liko wazi katika kupokea taarifa zinahusiana na jinai za rushwa rushwa ya ngono.
Amesema kuwa taarifa zinapotolewa zinalindwa kwa mhusika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...