Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV

VIDEO ya Msanii wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Nandy aliyeshirikiana na Mwana muziki kutoka DR Congo, Koffi Olomide ya ‘LEO LEO’ imetajwa kutoka hivi karibuni baada ya kibao chake (Audio) kuachiwa leo.

Meneja wa Msanii huyo wa Kike kutoka Tanzania, Moko Biashara amethibitisha hilo kupitia Michuzi Blog, Moko amesema Video ya Ngoma hiyo mpya ya Nandy aliyeshirikiana na Koffi Olomide itatoka hivi karibuni baada ya kuachiwa ‘Audio’.

“Kolabo ilikuwa siku nyingi lakini imefika muda tuiachie na Koffi ni mtu mkubwa kumpata kwake ni vitu tu vimefanyika na yeye anaweza kufanya kazi na mtu yeye,” ameeleza Moko

“Kufanya kazi na Koffi ni sawa sawa na kufanya kazi na mtu kama Jay Z, Menejimenti imekaa imeona ifanye kitu kama hicho”, amesema

Moko Biashara amesema mchango wa Serikali katika Sanaa ya muziki wa Tanzania ni kubwa, hiyo ni kutokana na ushirikiano wa bega kwa bega na Wasanii hao.

“Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Baraza la Sanaaa nchini (BASATA), Chama cha Hatimiliki Tanzania (COSOTA) na vyombo vingine vinashirikiana na sisi, wasanii kwa ukaribu sana”, ameeleza Moko.

Pia ametoa wito kwa wasanii wa Tanzania kufanya jitihada kwa hali na mali kuhakikisha wanafanikiwa na kuipeleka Tanzania mbali katika tasnia ya Sanaa


.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...