Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
WAJUMBE
wa Baraza la wadhamini la Chama Cha Mapinduzi ,(CCM) limewataka
viongozi wa vyama vya upinzani nchini kujiunga na Chuo cha uongozi na
Itikadi cha Mwalimu Nyerere ,kilichopo Kwamfipa,Kibaha,mkoani Pwani, ili
kujiongezea uwezo na kujifunza maadili na uzalendo wa nchi yao.
Walizungumza
hayo mara baada ya kukagua majengo ya chuo hicho,wakati
walipofanya ziara ya kutembelea chuo hicho ,kujionea maendeleo ya mradi
wa ujenzi wa chuo hicho.
Mwenyekiti
wa baraza hilo ,ANNA ABDALLAH na makamu wake PANDU OMARY KIFICHO
walisema, vyama imara kama CCM viongozi wake huandaliwa kuwa na maadili
na uzalendo hivyo hivyo chama chochote kinachotaka kujiimarisha basi
kipeleke viongozi na vijana wao kupikwa katika chuo hicho .
Hata
hivyo ,walielezea, baraza limeridhishwa na kukamilika kwa ujenzi huo
ambapo hatua iliyoko sasa ni kukamilisha kupitisha rasimu ya mitaala.
Anna
alishauri kuingiza somo uzalendo na maadili kwa wanafunzi watakaopikwa
katika chuo hicho hususani vijana waweze kujua historia ya nchi yao
PANDU OMARY KIFICHO ambae ni Makamu
mwenyekiti wa baraza hilo ,aliwataka vijana kujiunga na Chuo hicho ili
kupata mafunzo yatakayowapa maarifa watakapofanikiwa kuwa viongozi
kwenye ngazi mbalimbali.
Kwa upande wake,Naibu Katibu Mkuu, Rodrick Mpogoro alisema kuwa wataendeleza fikra za hayati Mwalimu Julius Nyerere.
""
Ambapo na ujenzi wa Chuo hiki unatekeleza kwa vitendo fikra hizo na
wanavyowaona viongozi waliotangulia wanapata faraja"aliongeza Mpogolo.
Msimamizi
wa mradi huo, EMANUELA KAGANDA ,alifafanua, mradi huo umekamilika kwa
upande wa Ujenzi wa majengo ,umegharimu kiasi cha sh.bilioni 90, na
kitakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 200.
Alisema
kuwa, ujenzi huo ulianza mwaka 2018, ambapo amedai umechelewa kutokana
na hali ya mvua pamoja na kuibuka kwa ugonjwa wa Covid-19 Corona.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...