Jane Edward,Michuzi TV, Arusha

WAJASIRIAMALI kutoka maeneo mbalimbali nchini  wameiomba serikali kutoagiza bidhaa hasa viungo kutoka nje ya nchi kwani tayari hapa nchini wanajitosheleza katika uzalishaji na ubora .

Waliyasema hayo  leo wakati wakizungumza katika maonesho ya nne ya mifuko na programu za uwezeshaji yanayofanyika  mkoani Arusha ambayo yanaenda sambamba na utoaji wa elimu mbalimbali kwa wajasiriamali.

Akizungumzia changamoto hiyo, Mjasiriamali kutoka wilaya ya Siha Roda Mshomi alisema kwa hapa Tanzania hivi sasa wamejitahidi  sana katika utengenezaji na uzalishaji  wa viungo na kuwa wanajitosheleza, hivyo ni vizuri watanzania wakatumia bidhaa za nyumbani hasa viungo badala ya kuagiza nje ya nchi.

Mjasiriamali mwingine,Athuman Abdalah kutoka wilayani Karatu ameiomba  serikali pia kutengeneza  mazingira rafiki ya upatikanaji wa vifungishio   ambavyo vimekuwa havipatikani kwa urahisi hapa nchini hadi nje ya nchi na inakuwa ni gharama sana kuvipata.

Katibu Mtendaji kutoka baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi, Beng'i Issa alisema kuwa, wajasiriamali wengi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinafanyiwa kazi huku akiwataka wajasiriamali hao kuhakikisha wanaboresha bidhaa zao ili ziweze kuendana na soko la ajira ndani na nje ya nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...