Mkuu wa mkoa wa Manyara  Joseph Mkirikiti akibadilishana mawazo na meneja masoko na ukuzaji biashara  Charles Magori  (aliyevaa miwani)kutoka  kampuni ya Sanlam Insurance alipotembelea banda hilo lililopo Katika maonyesho ya  nne ya mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayofanyika mkoani Arusha
Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha, Maximilian Matle Iranqe (kushoto) akiongea na Meneja wa HESLB - Arusha, Patrick Shoo kuhusu masuala mbalimbali ya utoaji wa mikopo kwa mwaka 2020/2021 alipotembelea banda la HESLB katika Maonesho ya Nne ya Mifuko na Program za Uwezeshaji yanayoendelea jijini Arusha.


 Na Woinde Shizza , Michuzi Tv-ARUSHA

JIJI la Arusha limefanya makubaliano ya kukutana na  mifuko ya programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi  Ili kuweza kujenga jukwaa la pamoja la kuwasaidia wajasiriamali.

Hayo ya yameelezwa na Mstahiki Meya wa jiji hilo Maximilan Iranq'e wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kutembelea  mabanda katika maonesho ya nne ya mifuko ya uwezeshaji wananchi kiuchumi yanayoendelea mkoani Arusha.

Alisema kuwa katika jukwaa hilo watahakikisha kwamba  wanawavuta wajasiriamali wote wadogo waliopo mtaani na kuwapa elimu pamoja na mikopo.

“ Kama serikali ina kila sababu ya  kuwasaidia wananchi waweze kuinua uchumi wao ambapo watapa elimu ya jinsi ya kufanya biashara na kuwapa mikopo Ili kuweza kukuza uchumi wao.” Alisema Meya.

Alisema serikali kuwa serikali inajukumu la kuwalinda wafanyabiashara wake, wajasiriamali na watu wanaoanzisha viwanda  ambapo suala la kuzuia bidhaa za nje litaaenda taratibu hadi bidhaa zinazozalishwa hapa nchini zitakapoweza kukidhi mahitaji.

“Tukisema leo tuzuie kila kitu kinachotoka nje sidhani Kama hawa wazalishaji wa ndani wanaweza kutosheleza soko na huwa serikali haikurupuki bali inafanya  utafiti kwanza,” Alieleza.

Aidha alisema kuwa maonesho hayo ni maonesho yanayohitajika sehemu mbalimbali za nchi kwani sehemu ambapo watanzania wanapata fursa ya kukutana na taasisi za kifedha pamoja na kujenga mtandao na wafanyabiashara wenzao.

Alisema kuwa wajasiriamali waliopo katika maonesho hayo ni wajasiriamali wazalendo na wanaothamini bidhaa za nyumbani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...