Na Woinde Shizza ,Michuzi Tv
Mganga
mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi amewataka wananchi kujenga tabia
ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa
ya kuambukiza pamoja na yale yasiyo ya kuambukizwa.
Aliyasema
hayo leo wakati akiongoza mazoezi ya pamoja akiwa na watumishi wenzake
kutoka Wizara ya Afya ,ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa pamoja na wananchi
wa jiji la Dodoma mazoezi yalifanyika katika uwanja wa jamhuri jijini
Dodoma.
Alisema kuwa
wananchi wengi wamekuwa na mazoea ya kukaa bila kufanya mazoezi jambo
ambalo linawasababishia kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara.
"Mazoezi
yanasaidia sana kuondoa magonjwa yasiyoambukiza kama sukari na presha
,pia huondoa usongo wa mawazo pamoja na kuleta mahusiano baina ya kundi
na kundi ,mtu na mtu au na jamii nzima na muunganiko wa kazi kupitia
mazoezi hayo"alibainisha Makubi.
Aidha
mbali na kufanya mazoezi mganga mkuu wa Serikali pia alishiriki katika
zoezi la uhamasisha wananchi kufanya usafi kwa kushiriki zoezi la
kufanya usafi wa mazingira katika uwanja wa Nyerere square.
Akiongea
wakati wa kufanya usafi huo amewataka wananchi kuimarisha usafi wa
mazingira ili kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...