WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt Dorothy Gwajima amewataka wanaume kutokalia kimya vitendo vya ukatili hasa pale wanapotendewa wao kwani itasaidia kujenga jamii yenye usawa.

Dk Gwajima ametoa kauli hiyo jijini Dodoma alipokua akitoa tamko kuhusu Vitendo vya Ukatili katika jamii mbele ya wandishi wa habari.

Dk Gwajima amesema vitendo vya ukatili vimezidi hapa nchini huku akitolea mifano mbalimbali iliyotokea hivi karibuni ya wanafamilia kufanyiana vitendo vya kikatili.

Amesema ukatili haufanywi kwa wanawake na watoto tu lakini hata kwa makundi mengine ikiwemo wanaume lakini wengi wao wamekuwa wakikaa kimya.

"Wanaume msione aibu, muache kukaa kimya dhidi ya vitendo vya ukatili mnavyofanyiwa. Toeni taarifa mapema kwa mamlaka husika muweze kupata msaada ili kuzuia madhara zaidi kutokea" Amesema Dk Gwajima.

Amezitaja sababu za ukatili huo ni pamoja na migogoro ya kifamilia ikiwemo kugombea mali, matatizo ya kisaikolojia na jamii kutotekeleza wajibu wake wa kutunza na kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya familia.

Dk Gwajima amesema Wizara itaendelea kuchukua jitihada zote kuhakikisha ukatili unatokomezwa kwa makundi yote, lakini jamii pia ina jukumu la kuwalinda makundi yote.

Aidha, amesema Wizara itaendelea kushughulikia mauaji ya wazee na kuwa haitorudi nyuma kupambana na ukatili wa aina yoyote ili nchi na mipaka yake ibaki salama kwa amani, upendo na kujiletea maendeleo.

Naye Afisa Ustawi Jamii Mkuu kutoka Wizara ya Afya, Amina Mafita amesema Wizara imejikita zaidi katika kuelimisha jamii kwa kuunda mabaraza kuanzia ngazi za vijiji na mitaa kwa lengo la kulinda makundi yote.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...