KATIKA kuadhimisha miaka 44 ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Dodoma Mjini umekabidhi misaada yenye thamani ya Sh. Milioni Moja kwa watoto wenye ulemavu wa akili na kuwatembelea wakina mama waliojifungua katika Hospitali ya Mkoa.

Misada iliyotolewa ni pamoja na  Juisi, Mchele, Pipi, Sukari, Mafuta ya kupaka, Miswaki na Madaftari

Akizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Katibu wa UWT Wilaya ya  Dodoma Mjini, Diana Madukwa amesema wameamua kufanya  mambo yanayogusa jamii pamoja na kuwatembelea  ili kujua changamoto zinazowakabili  na kuyafikisha mahali panapohusika.

“Katika kuadhimisha miaka 44 ya kuzaliwa kwa CCM tumeamua kwenda kutembelea watoto ambao wana ulemavu wa akili  na kuwapa msaada wakina mama ambao wamejifungua katika hospitali ya mkoa wa Dodoma kwasababu ni maeneo  ambayo yanayogusa jamii moja kwa moja," Amesema Madukwa.

Madukwa ameiasa jamii  kuwa na tabia ya kusaidia watoto waishio katika mazingira hatarishi na na wenye mahitaji maalumu huku akisisitiza jamii kuacha  tabia ya kuwanyanyapaa kundi hilo  kwani nao ni binadamu.

Amesema CCM ni chama tawala kinagusa kila tabaka na kuhakikisha kila mtu ambaye amezaliwa katika ardhi ya Tanzania anapata haki zake kulingana na maumbile yake.

“Serikali ya awamu ya tano imafanya jitihada kubwa kuhakikisha kila mwananchi anapata haki zake bila kujali maumbile yake hivyo serikali imekuwa ikitenga fedha kusaidia watu wenye mahitaji maalumu ili nao waweze kufikia malengo yake," Amesema Madukwa.

Kwa upande wake Muuguzi Mfawidhi Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Stanley Mahundo amesema katika kuadhimisha miaka 44 ya CCM jamii ikumbuke mchango wa chama hicho toka kingie madarakani.

Amesema Serikali ya awamu ya tano imekuwa mkombozi kwa wananchi kupitia sekta ya afya kwani imefanya uwekezaji mkubwa katika kuboresha na kuendeleza na jamii haina budi kukumbuka vitu kama hivyo.

“Serikali ya awamu ya tano imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya afya sasa ukija hospitali kila kitu kinapatikana hata zile rufaa zimepungua huduma muhimu zinapatikana kuanzia hospitali ya wilaya hiyo ni kazi nzuri iliyofanywa na serikali kupitia chama cha mapinduzi hivyo hatuna budi kukumbuka” Amesema Mahundo.

Naye mama aliyejifungua hospitali ya mkoa wa Dodoma sara matiko ameipongeza serikali kwa kuboresha huduma za mama mjamzito na aliyejifungua kwani sasa  huduma zimekuwa bora na za kuridhisha tofauti na zamani.

“Namshukuru sana Dk John Magufuli kiukweli sisi akina mama tunajisikia raha kutokana na huduma tunazopata kiukweli nchi imebadilika hata wafanya kazi wa hospitali wamekuwa na nidhamu tofauti na zamani,” Amesema.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...