KITUO cha msaada wa Sheria kwa Wanawake Tanzania (WLAC,) kimeendelea kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule za msingi kuhusiana na vitendo vya unyanyasaji na namna ya kukabiliana navyo.

Kupitia mradi wa Ulinzi kwa mtoto unaotekelezwa na WLAC kwa Shule kumi za Msingi katika Mkoa wa Dar es Salaam watoto wengi wamepata msaada dhidi ya vitendo vya ukatili walivyofanyiwa pamoja na elimu ya kuepukana na kuripoti matukio hayo.

Leo Februari 17, Timu ya WLAC imetembelea shule za Msingi za Tandika na Temeke na kutoa elimu kwa njia ya sanaa ili kuwalinda watoto.

Shule zinazonufaika na mradi huo ni pamoja na Shule  za msingi Tandika, Temeke, Mbagala, Kingugi, Mbaagala Annex, Mzimuni Magomeni, Kawe A, Mburahati, Tandale Magharibi na Hananasif.






Mratibu wa mradi wa Ulinzi kwa watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kutoka Kituo cha msaada wa Sheria Tanzania (WLAC,) Abiya Richard akitoa somo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Temeke,ambapo amewataka kutosita kuripoti matukio yoyote ya unyanyasaji, leo jijini Dar es Salaam.


 Mratibu wa mradi wa Ulinzi kwa watoto dhidi ya vitendo vya unyanyasaji kutoka Kituo cha msaada wa Sheria Tanzania (WLAC,) Abiya Richard akitoa somo kwa wanafunzi wa shule ya msingi Tandika,ambapo amewataka kutosita kuripoti matukio yoyote ya unyanyasaji, leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...